Jang'ombe Boys FC players who are
coaching by their new coach Said Kwimbi have been given a awakening of the
whole issue of football game discipline.
Speaking during the training of the team
today in training ground, Kwimbi has told the players that in order to become
successful in anything; they have to choose discipline as a compass and
direction toward that matter.
"My dear brothers, my children and
my friends, if you really have choosen football intentionally as a part of your
life, then make sure you switch on your discipline to the peoples, either
a young or an old, whether in the field during the exercise, during the match
and even you walking on the streets, because discipline is everything in the
human life, so even in the football game, you have to reserve it’s right in the
disciplinary matters, if you’ll do so then the football also shall
reserve your rights, and vice versa is true ".
"What I can say, this team
has been well decorated with great players, but I can assure you, in the
football even if you are a star, you can show how to kick the ball by using your
teeth, but if you are lacking in discipline you are nothing, the football
family recognizes the disciplinary player as their best player at all time, when
I’m talking about discipline doesn’t mean that you have to helps people carrying their loads on the streets only, no, but you have to follow Dos and Don’ts of Football"said Kwimbi.
Jang'ombe Boys FC will play its second
friend match since closing the Zanzibar transfer window, but for Coach Kwimbi
this is his first game since he took place as a coach of the club.
Jang'ombe Boys FC took this chance to
invites you all to this match to eyes witness yourelves our new talent
squard this season, the entrence fees is sh.1,000 / - and sh.2,000 / - only,
you are warmly welcome
KOCHA KWIMBI AAWAPA NASAHA
WACHEZAJI WA JANG'OMBE BOYS FC.
Wachezaji wa timu ya Jang'ombe
Boys FC ambao kwa sasa inafundishwa na kocha wao mpya Said Kwimbi wamepewa
nasaha juu ya suala zima la nidhamu ya mchezo wa mpira wa miguu.
Akizungumza wakati wa kufunga
mazoezi ya timu hio leo katika uwanja wa mazoezi wa timu hio, Kocha Kwimbi
amewaeleza wachezaji hao kwamba ili ufanikiwe katika kitu chochote basi ni
lazima nidhamu iwe ndio dira na kitu cha mbele katika kitu hicho.
"Ndugu zangu, watoto wangu
na marafiki zangu wachezaji, kama kweli nyinyi mmechaguwa mpira kuwa ni sehemu
ya maisha yenu, basi muhakikishe mnatunza nidhamu kwa wakubwa na wadogo, iwe
uwanjani wakati wa mazoezi, wakati wa mechi na hata mtaani, kwa sababu nidhamu
ndio kila kitu katika maisha ya mwanadamu, hivyo hata katika huu mpira wa miguu
basi unatakiwa kuutendea haki katika suala zima la kinidhamu, ukifanya hivyo
basi na wewe mpira utakutendea haki tu".
"Niseme timu hii
imebahatika kuwa na wachezaji wazuri sana, lakini nataka niseme hata uwe
"Star" unapiga mpira mpaka kwa meno lakini kama huna nidhamu basi
mchezaji wa maana, familia ya soka inamtambua yule mwenye nidhamu kuwa ndio
mchezaji bora, na ninapozungumzia nidhamu simaanishi kwamba ukiona mtu ukapokee
au umuamkie shikamoo au chei chei, laa hasha! nidhamu ya mpira
ni kuhakikisha kwanza unafanya yale walimu na timu inayataka na unayaacha yale
ambayo walimu na timu haiyataki" alisema Kwimbi.
Wachezaji, viongozi na wadau wakisikiza
nasaha za Mwalimu baada ya mazoezi.
Kuelekea mchezo wa kirafiki
kati ya Jangombe Boys FC na Villa United FC (Mpira Pesa) hapo kesho tarehe 21
Septembe 2017 saa moja za usiku katika Uwanja wa Amani, Kocha Kwimbi aliwataka
wachazaji wote 30 ambao wamesajiliwa na timu msimu huu kufika kwa wakati
klabuni ili timu nzima ifike pamoja kiwanjani kwa jaili ya mchezo huo wa
kirafiki.
"Nidhamu ni uwanja mpana
sana, hivyo nikizungumzia nidhamu basi ni pamoja na wachezaji wote thelathini
waliosajiliwa na timu na wanaohudhuria mazoezi, basi wote wafike mapema eneo
husika ili sote tuwepo pamoja kucheza mchezo huo, kwa sababu siku ya kesho
tunahitaji kuwatumia wachezaji wote, ili tuweze kurekebishana makosa na hatimae
tufanye vizuri katika ligi" alimalizia Kocha Kwimbi.
Jangaombe Boys FC itacheza
mchezo wake huo ukiwa ni wa pili tangu dirisha la usajili kufungwa, lakini
utakuwa ni mchezo wa mwanzo kwa Kocha Said Kwimbi tangu achukuwe mikoba ya
kuinoa timu hio.
Jang'ombe Boys inawakaribisha
nyote kuja kuona kikosi chetu kipya kilichosheheni kila aina ya vipaji msimu
huu, kiingilio ni sh.1,000/- na sh.2,000/-.


Maoni
Chapisha Maoni