PAZIA LA LIGI KUU ZANZIBAR 2017/2018 LAFUNGULIWA KWA NGAO YA HISANI

Timu ya Miembeni City, ambayo ilipanda daraja kwa kumaliza ligi ya daraja la kwanza taifa 2016/17 kwa kushika nafasi ya kwanza, watafungua pazia la ligi kuu ya Zanzibar (Zanzibar Premier league) kwa kucheza mchezo maalum wa ngao ya hisani ya jamii, ambapo katika mchezo huo watamenyana na mabingwa wa ligi kuu Zanzibar 2016/17 JKU.

Mabingwa hao wa ligi daraja la kwanza Taifa (Miembeni City) na  Mabingwa wa Ligi kuu ya Zanzibar (JKU) watakutana siku ya Jumanne Septemba 19, mwaka huu katika dimba la Uwanja wa Amaan kwa mujibu wa taarifa kutoka ZFA.

Kumalizika kwa mchezo huo wa ngao ya hisani ya Jamii ni kuashiria kwamba pazia la Ligi Kuu soka Visiwani Zanzibar limefunguliwa rasmi, ambapo hivi sasa vilabu vyote vitakavyoshiriki ligi kuu msimu huu, viko mafichoni kufanya maandalizi ya mashindano hayo tukiwemo sisi Jang'ombe Boys FC, mashindano ya mwaka huu yanaonekana yatakuwa na ushindani wa hali ya juu sana kutokana na kila timu kuamini kwamba wamefanya usajili wa wachezaji wazuri zaidi.

Nyote mnakaribishwa!


THE ZANZIBAR PREMIER LEAGUE 2017/18 TO START WITH COMMUNITY SHIELD CLUSH.



Miembeni City FC, who promoted after completing at the 1st position of the 2016/17 Zanzibar first Division on the national level league, will open the Zanzibar Premier League league by playing the special Comunity Shield game ,  this game will be versus  Zanzibar Premier League champions 2016/17 JKU.

Zanzibar Premier League (JKU) Champions League will meet with Zanzibar first Division's Champions (Miembeni City)Tuesday, September 19, this year at the Amaan Stadium, according to  statement from ZFA official.

The end of this Community Shied clush clearly states that, the Premier League scenes in Zanzibar Island has been officially opened, where all the clubs will share the Premier league this season are at the hiding places for the preperation of the tournament including Jang'ombe Boys FC, this season competition seems to be much competitive, due to each club of the premier league believes has sign the best players.

You are mostly welcome!

Maoni