RAIS WA JANG'OMBE BOYS AMLILIA MCHEZAJI WA ZAMANI MZEE MAJHAM

Rais wa timu ya jang'ombe Boys FC Ali Othman 'Kibichwa' amehuzunishwa na kifo cha aliyekuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar, timu yataifa ya Tanzania, klabu ya Vikokotoni, klabu ya Cosmo na vilabu nyenginevyo vikiwemo vya (hockey) mpira wa magongo na riadha na michezo mengineyo.


Rais wa Jang' ombe Boys 

Akizungumza na matandao huu mapema asubuhi mara baada ya kupata taarifa ya kifo cha mkongwe huyo kibichwa amesema.

"Binafsi yangu nimezipokea taarifa hizi kwa mshtuko mkubwa sana, kwani niseme sasa wanasoka, wanariadha na wana mchezo wa magongo tumekosa sehemu ya kukimbilia kuchukuwa maarifa ya michezo hii.

"Historia inamtambuwa Marehemu mzee Abdul Majham Omar, kwa kazi kubwa aliyoifanya katika michezo na kuitambulisha nchi yetu ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, kwani marehemu alikuwa na vipaji vya michezo tofauti, marehemu amecheza mpra wa miguu katika timu ya taifa ya zanzibar, Tanzania na pia ametumikia vilabu vya Cosmo, vikokotoni na vilabu vyenginevyo.




"Mambo mengine ya Marehemu sikuwa nikiyajuwa, lakini nimeyapata baada ya msiba wake kwamba pia alikuwa mwana riadha pamoja na huo mchezo wa magongo (Hockey) na kwa mchezo huo pia alitumikia timu zote mbili za taifa yaani Zanzibar na Tanzania"

"Hivyo kwa niaba ya washabiki, wachezaji, wanachama na wapenzi wote wa Jangombe Boys nasema tunaungana na ndugu jamaa na marehemu katika msiba huu, tunamuomba Allah ampokee mzee wetu kwa mapokezi ya salama, amjaalie nuru kabuni mwake na amsamehe dhambi zake zote, na tunaombea wafiwa wote mioyo ya subra katika kipindi hichi kigumu cha msiba - Amiin" alimalizia Kibichwa.

Innaa lillahi wainnaa ilayhi raajiuun.

Maoni