'Ahadi ni deni' huu ni msamiati makhsusi ambao hutumika mara nyingi pale mtu anapoahidi kufanikisha jambo fulani, hivyo kwa kutumia msamiati huo hakuna shaka yule anaeahidiana na mwenzake jambo fulani basi huwajibika kutimiza lile aliloahidi, na unapotimiza huwa umeonyesha kiwango cha juu cha uungwana.
Naam, hakuna shaka kwa wapenzi, wadau, wanachama na wapenzi wa Jang'ombe Boys wote watakubali kwamba Khamis Mussa 'Rais' ametimiza ahadi aliyoitoa kwao juzi tarehe 02 Oktoba 2017 kabla ya mchezo wetu wa jana dhidi ya KMKM, alipokuwa akihojiwa na mtandao huu Rais aliahidi kuwafungia goli KMKM na kusisitiza kwamba hakuna wa kumzuia asifunge goli.
Hivyo kitendo cha Khamis Mussa 'Rais' ni kuonyesha kwamba yeye ni hodari na ni muungwana kwa sababu aliweka ahadi ya kufunga goli na hatimae kweli amefunga pamoja na kukabwa sana na kuchezewa rafu na mabeki wa KMKM.
Mkwaju maridadi aliolenga golini mwa KMKM na kumpita golikipa wa KMKM kama umeme ulitosha kuifanya mechi hio kumalizika kwa sare ya goli 1-1 na kuifanya timu yetu ianze ligi kwa kuvuna alama moja.
Nae Rais amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia uzima na utimamu wa mwili na ajili kitu kilichomfanya afunge goli ambalo aliwaahidi washabiki kama atawafungia.
"Kiukweli nimefarijika na kufurahi sana, baada ya kufunga goli kwa sababu nilishawaahidi washabiki na timu kwa ujumla hivyo naahidi nitaendeleza wimbi hilo la kufunga magoli na hatimae kuisaidia timu kufanya vizuri" alisema Rais.
Ikumbukwe kwamba Khamis Mussa 'Rais' aliwafunga KMKM katika mchezo wa ligi kuu iliyomalizika mzungo wa kwanza, ambapo tulishinda 2-0 na goli la pili likafungwa na Abrahmani Othman 'Chinga'.

Maoni
Chapisha Maoni