Kocha msaidizi wa Jang’ombe Boys Issa Othman ‘Amasha’
amesema timu yake ipo tayari kwa pambano la keshokati ya timu yake dhidi ya wazamiaji wa KMKM,
hii ni kutokana na kwamba asilimia kubwa ya wachezaji wako na afya njema na
wachezaji wawili tu ndio ambao ndio majeruhi kati ya wachezaji 30 wa timu hio,
akizungumza na mwandishi wa mtandao huu kocha Amasha amesema ni wachezaji
wawili tu ndio ambao ni wagonjwa.
“Tumemaliza kufundisha timu yetu na sasa kilichobaki ni
wachezaji kuonyesha kwa vitendo kile tulichokuwa tukiwafundisha mazoezini, na
hio ndio kazi moja kubwa ya mwalimu a mpira, nakiamini kikosi chetu kwani
kimeonyesha uezo wa juu katika mechi za kirafiki tulizocheza.
“Wachezaji wako vizuri, wana ari, wameshazoeana na kuishi
kwa maelewano ya hali ya juu sana ndani na nje ya uwanja sambamba na kuwa na
mshikamano wa hali ya juu, pia nashukuru kwamba hatuna majeruhi wengi katika
timu, tuna wachezaji watatu tu ambao ndio wana majeraha ambayo yametufanya
tusiweze kuwatumia kwa mchezo wa kesho, ambao ni Hassan Choum, Shomari Abdallah Almas na
Abubakar Mkubwa (Kamara).
"Kuhusu ugumu wa mchezo huo, ni kweli nakiri mchezo utakuwa mgumu sana na wa ushindani, lakini niseme KMKM wanatufahamu sisi na sisi vile vile tunawafahamu, lakini niseme nina matumaini matumaini makubwa ya ushindi kwa mchezo wa kesho 'In shaa Allah'.
"Kuhusu ugumu wa mchezo huo, ni kweli nakiri mchezo utakuwa mgumu sana na wa ushindani, lakini niseme KMKM wanatufahamu sisi na sisi vile vile tunawafahamu, lakini niseme nina matumaini matumaini makubwa ya ushindi kwa mchezo wa kesho 'In shaa Allah'.
“Kuhusu Abdi Kassim (Babi) ni kweli hakuhudhuria mazoezi
leo, lakini tunazosababu za kutohudhuria kwake, lakini hata hivyo atakuwepo
kesho katika mechi, hivyo benchi laufundi linaweza kuamua kumtumia kwa sababu
ni mchezaji halali wa timu hii.
“Kiujumla wachezaji wote, ambao wamehudhuria mazoezi tangu
yafunguliwe rasmi, wako vizuri kiafya na kiakili ya mchezo, hivyo sisi walimu
ndio wapangaji wa timu na tumeshafanya tathmini ya wachezaji ambao wanafaa
kutumika katika mchezo wa kesho, kwa sababu mchezo wa mpira una idadi maalum ya
wachezaji, basi tutachagua wachezaji wa kesho na waliobaki watacheza mechi
nyengine, hii ni mechi moja lakini ziko nyingi zinakuja” Alisema Amasha.
Jang'ombe Boys itajitupa uwanjani kusaka alama tatu muhimu za kufungulia msimu mpya wa ligi kuu ya Zanzibar huku ikiwa imeengeza nguvu kwa kusajili wachezaji wapya 8 na kuondoa wachezaji watatu pekee huku ikihakikisha inamrejesha mshambuliaji wake aliyekuwa katika klabu ya Singida United Abdahmani Othaman (Chinga) ambaye pia alikuwa akiwaniwa na klabu ya KMKM ambao ndio wanaopmbana nao kesho alasiri katika kiwanja cha Aman mjini Zanzibar.
KILA LA KHERI WASTAARABU WA NG'AMBU

Maoni
Chapisha Maoni