Ligi kuu soka Visiwani Zanzibar kanda ya Unguja ilianza kutimua vumbi mnamo tarehe 03//10/2017 michezo miwili ilichezwa katika uwanja wa Amaan.
Saa 8 za mchana mabingwa watetezi wa JKU walianza vyema utetezi wao kwa kuichapa Mafunzo bao 1-0 kwa bao lililofungwa na Ali Haji Said maarufu Zege dakika ya 44.
Baadae saa 10 jioni Jangombe Boys na KMKM wakatoka sare ya 1-1.
KMKM bao lao lilifungwa na Salum Akida dakika ya 5 na bao la Jang'ombe Boys likafungwa na Khamis Mussa (Rais) dakika ya 25.
Michezo ya tarehe 04/10/2017:
Kilimani City 3-1 Kipanga.
KVZ 1-) Charawe
Michezo ya tarehe 05/10/2017
Polisi 1-0 Miembeni City.
Zimamoto 1- 0 Taifa ya Jang'ombe
Leo kutakuwa na mchezo kati ya Black Sailor vs Chuoni saa 10.00 alasiri.

Maoni
Chapisha Maoni