MCHEZAJI KINDA WA JANG'OMBE BOYS APEWA 'BIG UP' NA KOCHA KWIMBI


Mchezaji kinda wa Jang'ombe Boys Yakoub Amour Bakari amemfurahisha kocha wake Said Kwimbi kwa kiwango cha hali ya juu alichokionyesha wakati Jang'ombe Boys ilipochuana na KMKM jana katika kiwanja cha Amani katika mchezo wa mwanzo wa ligi kuu ya Zanzibar mzunguko wa kwanza.


Mchezaji Yakoub Amour


Yakoub ambaye pia alikuemo katika kikosi cha timu ya wilaya ya mjini ambayo ilichukuwa ubingwa wa 'Rolling Stone' ya vijana walio chini ya miaka 17, Yakoub jana alipangwa kucheza beki ya kulia namba ambayo kikawaida huchezwa na Shomari Abdalla aliye majeruhi kwa sasa.

Yakoub alicheza vizuri nafasi hio licha ya umri wake mdogo, lakini alionyesha umahiri na uwezo wa hali ya juu, na ndiye aliyekuwa akipeleka mashambulizi ya hatari langoni mwa KMKM na hatimae kusababisha goli la kusawazisha lililofungwa na Khamis Mussa Rais.

Akizungumza mbele ya mtandao huu kocha kwimbi baada ya mechi hiyo, kocha Kwimbi alimpongeza Yakoub kwa kazi nzuri sana aliyoifanya licha ya udogo wake wa umri.

"Nataka nimpongeze kwa dhati mchezaji mdogo kabisa Yakoub kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya, Yakoub Kesho Insha Allah ntakuletea zawadi, na nikwambie ukiendelea kujituma nakuahidi timu ya Taifa ya Zanzibar unaitwa, sina wasi wasi na wewe endapo utajituma" alisema Kocha Kwimbi.

Akizungumza na mtandao huu Yakoub amesema anamshukuru mwalimu kwa kumpa nafasi ya kucheza katika mechi hiyo ngumu na hatimae kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wake na baadae Mwalimu kuridhika na kazi aliyoifanya.

"Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia uzima wa afya, pili nimshukuru yeye Mwalimu kwa mafunza aliyonipa tangu aanze kunifundisha, tatu nimshukuru kwa kuniona na kuniamini kwamba naweza kuitumikia nafasi hio na hatimae kufanya yale mazuri niliyoyafanya.

"Namshukuru sana kwa kuikubali kazi yangu pia kufikia hatua hadi kunisifia katika hadhara ya watu, niseme hio ni changamoto kwangu naahidi sitovimba Kichwa na kulewa sifa, bali nitazidisha juhudi katika mazoezi ili nijihakikishoe namba ya uhakika katika kikosi" alisema Yakoub

Hivyo Yakoub atakabidhiwa zawadi yake leo kiwanjani na Kocha Said Kwimbi kiwanjani, fika ushuhudie tukio hilo, kwa naiba ya waandishi wa mtandao huu unampongea mchezaji kinda Yakoub na unaahidi kumzawadia pia.


Maoni