NUKUU MUHIMU KWA WACHEZAJI.

“Katika maisha lazima ujue kitu gani kinatakiwa katika kazi yako, ukishajua huwezi kupata tabu. Miiko ya mpira inajulikana lakini kikubwa ni kupumzika tu”  kiungo mkongwe wa Kagera Sugar George Kavila


                       George Kavila (kushoto) akikabiliana na Elias Maguli 
                            desemba 26 mwaka 2015 Simba wakichapwa 1-0.

Nukuu hio aliitoa alipokuwa akihojiwa na mtandao wa Shaffih Dauda, wakati alipohijiwa ni kwa nini amedumu katika soka kwa muda mrefu.

Mkongwe huyo wa ligi kuu Tanzania bara na nahodha wa Kagera Sugar ameanza kucheza ligi mwaka 1998 akiitumikia Coastal Union ya Tanga ambayo ndio timu yake ya kwanza kumtambulisha kwenye soka kwa ngazi ya juu nchini, tangu mwaka huo hadi sasa bado anacheza ligi kuu ya Vodacom.

Kuna kila sababu wachezaji wa Zanzibar kujifunza kwa wakongwe kama hawa.

Maoni