Tunamshukuru Mungu Kwa kutuwezesha kutuweka na neema hii ya uhai na uzima, na hii si kwa ujanja wetu bali ni kwa neema na ihsani zake Mwenyezi Mungu, kwani wapo wajanja wa wajanja ulimwenguni lakini ujanja wao wote umekwisha na sasa wanahemea ndani ya matumbo ya ardhi.
Lengo ni kuwashukuru sana na zaidi ya sana nyote mnaotembelea Blogu yetu ya Jang'ombe Boys FC, kwani zipo blogu nyingi ambazo ni nzuri zaidi ya hii lakini mmeamua kuziwacha zote hizo na kuamua kufatilia kwa ukaribu Blogu hii, hvyo tunawashukuru na tunaomba muendelee kuifatilia zaidi na zaidi.
Kiukweli ni muda mchache sana tangu blogu hii kuanzishwa lakini imeonekana kuwavutia wengi sana na ndio maana imevuna wafuatiliaji wengi, blogu hii imeanzishwa mwezi wa Septemba 14,2017 ni mwezi mmoja kasoro siku nne lakini ina jumla ya wasomaji 1174 ambao wanatoka nchi mbali mbali duniani zikiwemo:
S/N
|
NCHI/COUNTRY
|
IDADI
YA WAFATILIAJI/VIEWERS
|
1
|
TANZANIA
|
1061
|
2
|
UK –
UINGEREZA
|
19
|
3
|
TURKEY
|
19
|
4
|
KENYA
|
15
|
5
|
CANADA
|
14
|
6
|
UAE -
ARABUNI
|
13
|
7
|
LIBYA
|
10
|
8
|
USA
|
10
|
9
|
GERMANY
|
7
|
10
|
IRELAND
|
6
|
TOTAL
|
1174
|
Hii inaonyesha ni jinsi gani inavyofatiliwa na kupendwa ulimwenguni, hivyo nakusihi wewe mshabiki wa timu yetu kuzisambaza taarifa rasmi za timu yetu kwa njia mbali mbali unazoziamini, lakini tunakuomba uisambaze blogu hii na kurasa pamoja na kuta setu zote za Jang'ombe Boys.
Hivyo kuanzia sasa unaombwa na wewe kweka (share) blogu hii katika ukuta wako wa facebook kila siku ili kuengeza wafuatiliaji wengi zaidi, kwa kuwa kila tukipata wafatiliaji wengi tunaamini kuna fursa nzuri mbeleni zinaweza kujitokeza katika kuhakikisha Jang'ombe Boys inakwenda mbele zaidi ya hapa ilipo sasa.
Tunawathamini nyote kwa kutuunga mkono na tu naamini uungaji wako mkono ndio mafanikio ya timu yetu.
Tunawathamini nyote kwa kutuunga mkono na tu naamini uungaji wako mkono ndio mafanikio ya timu yetu.
Maoni
Chapisha Maoni