Timu yetu ya Taifa ya soka ya kisiwa cha Zanzibar (Zanzibar Heroes) imeshasili nchini Kenya Salama usalimini kama tulivyoelekeza dua zetu juu ya hilo sambamba na kukabidhiwa ratiba ya mashindano ya CECAFA Cup na waandaaji wa mashindano hayo.
Katika ratiba hio iliyokabidhiwa na baadae kuanikwa hadharani na chama kinachosimamia na kuongoza mpira wa miguu Zanzibar ZFA inaonyesha kwamba Zanzibar Heroes ipo kundi moja na Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi), Kenya, Tanzania (Kilimanjaro Star) na Libya.
Zanzibar Heroes itashuka dimbani kuanza ratiba yake kwa kucheza mchezo na timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi), ieleweke kwamba mchezo huu ni mgumu sana kwetu, kwa sababu katika mashindano kama haya ya CECAFA yaliyofanyika mwaka 2012 nchini Uganda, jioni ya tarehe 29/11/2012 Zanzibar Heroes iliweza kung’ara baada ya kuichapa timu ya taifa ya Rwanda “Amavubi” kwa mabao mawili kwa moja katika mchezo wa kundi C katika mwendelezo wa mashindano ya Cecafa Tusker Challenge Cup 2012.
Alikuwa ni kiungo mahiri wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ ambaye, magoli yake mawili yaliipa Zanzibar ushindi wa 2-1 dhidi ya Rwanda, katika mchezo wa Kundi C, mchezo ambao ulifanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, jijini Kampala.
Vialli alifunga mabao yake moja kila kipindi, la kwanza dakika ya sita na la pili dakika ya 61, yote akionyesha yeye ni fundi na mwenye akili na maarifa ya soka kutokana na kutulia na kumtungua kipa hodari kabisa katika ukanda huu kwa wakati ule, Jean Claude Ndoli.
Rwanda ilipata bao lake kupitia kwa Dadi Birori dakika ya 79, ambaye aliingia uwanjani dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Tumaine Ntamuhanga.
Ushindi huo, Zanzibar Heroes ilipata matumaini ya kwenda Robo Fainali ya michuano hio, ikipanda kileleni mwa Kundi hilo, kwa pointi nne, Rwanda ikishuka hadi nafasi ya pili kwa pointi zake tatu, sawa na Malawi, wakati Eritrea ikashika mkia kwa pointi yake moja.
Hivyo katika mashindano ya mwaka huu ya CECAFA Rwanda watarudi kiwanjani siku ya tarehe 05/12/2017 kupambana na Zanzibar Heroes huku ikiyakumbuka majeraha waliyoyapata kutoka kwa Zanzibar Heroes miaka mitano iliyopita, ni dhahiri watapania kuzuia matokeo kama yale yasijirejee.
Kuna haja kwa majeshi wetu tuliowatuma wa Zanzibar Heroes, kulifahamu hili kwamba sisi ni wababe kwa Rwanda katika mashindano hayo na tunataka kudumisha ubabe wetu huo kwa kuwafunga tena vijana wa 'Amavubi' ili kubakisha heshima yetu nchini Rwanda, mbali ya hivyo wachambuzi wengi wa soka wa Afrika Mashariki wanaliona kundi hilo la Zanzibar Heroes kuwa ni kundi la kifo katika mashindano hayo, hivyo endapo tukipambana katika mchezo huo na tukapata ushindi basi tutakuwa tumejiweka katika mazingira mazuri na Salama katika kundi hilo.
Kwa niaba ya wadau wote wa mtandao huu tunaitakia Zanzibar Heroes mchezo mwema na wenye matokeo ya ushindi mnono katika mchezo huo.
Kikosi cha Zanzibar Heroes kilichowalaza Wanyarwanda 2-1 mwaka 2012
Katika ratiba hio iliyokabidhiwa na baadae kuanikwa hadharani na chama kinachosimamia na kuongoza mpira wa miguu Zanzibar ZFA inaonyesha kwamba Zanzibar Heroes ipo kundi moja na Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi), Kenya, Tanzania (Kilimanjaro Star) na Libya.
Zanzibar Heroes itashuka dimbani kuanza ratiba yake kwa kucheza mchezo na timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi), ieleweke kwamba mchezo huu ni mgumu sana kwetu, kwa sababu katika mashindano kama haya ya CECAFA yaliyofanyika mwaka 2012 nchini Uganda, jioni ya tarehe 29/11/2012 Zanzibar Heroes iliweza kung’ara baada ya kuichapa timu ya taifa ya Rwanda “Amavubi” kwa mabao mawili kwa moja katika mchezo wa kundi C katika mwendelezo wa mashindano ya Cecafa Tusker Challenge Cup 2012.
Vialli alifunga mabao yake moja kila kipindi, la kwanza dakika ya sita na la pili dakika ya 61, yote akionyesha yeye ni fundi na mwenye akili na maarifa ya soka kutokana na kutulia na kumtungua kipa hodari kabisa katika ukanda huu kwa wakati ule, Jean Claude Ndoli.
Rwanda ilipata bao lake kupitia kwa Dadi Birori dakika ya 79, ambaye aliingia uwanjani dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Tumaine Ntamuhanga.
Hivyo katika mashindano ya mwaka huu ya CECAFA Rwanda watarudi kiwanjani siku ya tarehe 05/12/2017 kupambana na Zanzibar Heroes huku ikiyakumbuka majeraha waliyoyapata kutoka kwa Zanzibar Heroes miaka mitano iliyopita, ni dhahiri watapania kuzuia matokeo kama yale yasijirejee.
Kikosi cha Zanzibar Heroes cha mwaka 2017
Kwa niaba ya wadau wote wa mtandao huu tunaitakia Zanzibar Heroes mchezo mwema na wenye matokeo ya ushindi mnono katika mchezo huo.

Maoni
Chapisha Maoni