BANDA: NAWAAHIDI MAMBO MAZURI

Mchezaji Hassan Seif (Banda) ambaye amesajili na timu yetu akitokea Taifa ya Jang'ombe, yenye maskani yake katika mtaa wa Urusi Jimbo la Mpendae amesema, kwa sasa ameamua kujiunga na timu ya Jang'ombe Boys FC kwa sababu ni timu anayoendana nayo, Banda ameyasema hayo uwanja wa Amani wakati akihojiwa na waandishi wa habari baada ya mchezo kati ya Jang'ombe Boys na Shaba FC ambapo Jang'ombe Boys ilishinda goli 4-0.

Banda akizungumza na mwandishi
Wa habari.

"Kwa sasa mimi ni mchezaji halali wa Jang'ombe Boys nikitokea Taifa ya Jangombe, nimeamua kuja hapa kwa sababu nimeona kwamba hii ni timu ninayoendana nayo, hivyo nawashukuru viongozi, wanachama, wapenzi na wachezaji wenzangu kwa kunipokea mapokezi mazuri, mapokezi ambayo ni kistaarabu kabisa ambapo baadhi ya timu hawana ustaarabu kama huo".

"Kwa sasa tunasikiliza maelekezo na mafunzo ya walimu,  tunayachukuwa na tunayafanyia kazi ili kuiletea ushindi timu yetu, kitu ambacho ndio matarajio ya kila mdau wa timu, kuanzia sisi wachezaji, makocha, viongozi, washabiki na wanachama, ingawa mpira una matokeo matatu lakini kwa jinsi timu yetu ilivyosheheni wachezaji wazuri na wenye vipaji basi kwa niaba ya wachezaji wenzangu nawaahidi kuwaletea matokeo mazuri katika msimu wa ligi itakaoanza hapo Oktoba 3" alisema Banda.



Nao washabiki wa timu kwa upande wao wanaipongeza kamati ya usajili wa timu iliyoongozwa na kocha msaidizi wa timu Issa Othman (Amasha) kwa usajili bora kabisa, ambapo wamesifu uwepo wa wachezaji wakongwe na wenye uzoefu wa muda mrefu na kusema utaleta mafanikio katika timu kwa sababu wachezaji wachanga watajiufunza mambo mengi kutoka kwao na hatimae kuisaidia timu kupata matokeo mazuri.


Maoni