RAIS WA JANG'OMBE BOYS AFUNGA HAT-TRICK YA PILI YA LIGI KUU ZANZIBAR 2017/2018

Dakika 3, 19 na 20 zilitosha kwa Khamis Mussa "Rais" kuifungia Jang'ombe Boys goli tatu na kufanya aingie katika orodha ya wachezaji waliofunga "hat-trick".

Mshambuliaji Khamis Mussa 'Rais' baada ya kukabidhiwa mpira wake.

Hii ni "hat-trick ya pili tangu ligi kuu ya Zanzibar ianze katika msimu huu wa 2017/2018, ambapo hat-trick ya kwanza ilifungwa na mchezaji Salum Akida wa KVZ, hivyo ni kusema mpira wa pili wa ligi kuu Zanzibar kuondoka katika milki ya ZFA na kuhamia katika milki ya wachezaji waliofunga goli tatu tatu katika mechi moja.

Katika mchezo huo Jang'ombe Boys FC walifakiwa kiwafunga Charawe FC kwa jumla ya magoli 4-2, ambapo goli la 4 lilifungwa na Hafidh Barik aliyeingia kuchukuwa nafasi ya mshambuliaji mwenzake Abdalla Idd (pina) aliyesajiliwa kutokea Gulioni FC.

Maoni