Jang'ombe Boys FC baada ya kucheza michezo mitatu ya kirafiki sasa kucheza na timu ya jeshi ambayo pia inashiriki ligi kuu ya Zanzibar, ikumbukwe kwamba ligi kuu ya Zanzibar inashirikisha timu za kijeshi/vikosi zaidi ya nne, miongoni mwao ni Kipanga.
Akiuambia mtandao huu kocha msaidizi wa Jang'ombe Boys Issa Othman (Amasha) amesema kwamba ni vyema tukajipima nguvu pia na timu za kijeshi kwa sababu na wao ni wapinzani wetu katika ligi.
Kocha 'Amasha' akizungumza
na mwandishi wa habari.
"Maamuzi hayo tuliyafanya kwa sababu timu za kijeshi ni timu ambazo, tunashindana nazo katika ligi na ni timu ngumu kiukweli katika ligi, hivyo tukaona ni vyema tucheze na japo timu moja miongoni mwa hizo ili tusome na tujifunze kucheza na timu hizo za vikosi" alimalizia Amasha.
Kikosi cha Kipanga FC msimu 2016/17
Hivyo mchezo huo utapigwa siku ya Jumanne ya tarehe 26/09/2017 katika kiwanja cha Amani saa moja ya usiku, kiingilio ni 1000/- na 2000/-.
Njooni muburudike.
Maoni
Chapisha Maoni