BOYS WAINYANYASA TAIFA YA JANG'OMBE

Timu yetu  Jang'ombe boys imeendeleza wimbi lake lake la  ushindi mbele ya Watani wetu Taifa ya Jang'ombe baada ya kuwafunga mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar uliopigwa jana jioni katika uwanja wa Amaan.

Shukrani zetu kwa Hafidh Barik (Fii) kwa ktufungia goli dakika ya 6 ya mchezo na Juma Ali (Mess) dakika ya 66.


Kwa matokeo hayo rikodi yetu ya kuwafunga wakombozi bado iko juu,  baada ya kukutana mara 8 katika historia huku mara 5 tukishinda, mara 2 tukafungwa.

Msimu huu wa mwaka 2016-2017 tumekutana Novemba 19, 2016 katika Bonanza la Coconut FM ambapo matokeo Taifa 2-0 Boys, mabao ya Taifa yalifungwa na Baraka Ushindi na Mohd Said “Mess.

Disemba 10, 2016 tulikutana kwenye Ligi kuu soka ya Zanzibar Mzunguko wa kwanza na mataokeo Mkombozi 2-2 J. Boys, mabao ya Taifa siku hiyo alifunga Omar Yussuf Chande dakika 9 na Abdallah Mudhihir (Mido) dakika 60 wakati mabao ya yetu yote alifunga Khamis Mussa (Rais) dakika ya 45 na 53.

Disemba 30, 2016 pia tulikutana tena kwenye Kombe la Mapinduzi 2017 na matokeo Taifa 1-0 J. Boys kwa bao pekee lililofungwa na Hassan Seif “Banda”.

Tulikutana tena Aprli 25, 2017  katika ligi kuu soka ya Zanzibar Mzunguko wa pili hatimae tukapata ushind wa 1-0 Boys, bao pekee lililofungwa na Khamis Mussa “Rais”.



Mnamo mei Mei 14, 2017 katika ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora Mzunguko wa kwanza tukawala Taifa 0-3 Boys mabao yetu yalifungwa na Khamis Mussa “Rais”, Khatib Ng’ombe alijifunga mwenyewe na Juma Mess la tatu.

Jumapili ya July 30, 2017 kwenye mzunguko wa pili ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora tulikutana tena ambapo tulishinda 2-0 kwa mabao ya Hafidh Barik (Fii) dakika ya 6 na Juma Ali (Mess) dakika ya 66.


Mwaka 2012-2013 tukiwa daraja la pili wilaya ya mjini tuliwafunga Taifa mara mbili, tuliwafunga 2-1 kwenye ligi hiyo, na katika Kombe la Waamuzi  tena tukapata ushindi baada kushinda kwa penalti 5-4 kufuatia dakika 90 kumalizika bila kufungana 0-0.

Maoni