'FINI' OF JANG'OMBE BOYS FC HAS ENTERTAINED THE 'HEARTS & SOULS' OF FOOTBALL STAKEHOLDERS.




Jang'ombe Boys FC's player who signed  this season from Kilimani City named Helfini Salum, tonight has entertain the hearts and Souls of football fans and stakeholders, who get chance to watch the friendly match between our team versus Villa United (Mpira Pesa).

Helifini Salum appeared to own the best in the middle field position and became one of the players who gave great support to ensure his team well manage the 3-5-2 system and made Villa United players unable to understand each other.

Even IF the clash ended with the draw results, but is Jang'ombe Boys FC who get many chance of reaching  to Villa United goalkeeper and missed all the opportunities they had received.

Due to his both ability and Courageous, coach panel that was closely proximity to the match, the panel led by coach Hemedi Morocco, together they decides on our player Helfini Salum as the "Man of the Match".

Do not miss to came again at Amani Stadium this Sunday night, witnessing another Jang'ombe Boys FC  friendly game between Jang'ombe Boys FC versus Shaba FC from Kojani Pemba.

Tafsiri kwa kiswahili:

'FINI' WA JANG' OMBE BOYS AZIKONGA NYOYO ZA WADAU WA SOKA ZANZIBAR.

Mchezaji wa Jang'ombe Boys FC aliyesajiliwa na timu hii msimu huu akitokea Kilimani City Helfini Salum, usiku wa leo alizikosha nyoyo za wadau wa soka waliokuepo Kiwanjani hapo.
Helifini almaarifu Fini, alionesha umahiri na uhodari mkubwa na kuimiliki vyema nafasi ya kiungo na kuwa miongoni mwa wachezaji waliotoa msaada mkubwa kuhakikisha wanaumudu mfumo wa 3-5-2 na kuwafanya wachezaji wa Villa United washindwe kuelewana na kujikuta wakilinda zaidi kuliko kushambulia.

Mchezaji Helfini Salum 'Fini' mbele ya
kocha 'Morocco' akipokea Zawadi.

Pambano hilo lilimalizika kwa timu hizo kutoka suluhu bila kufungana, lakini ni Jang'ombe Boys FC ndio waliofika golini kwa Villa United na kukosa nafasi zote ambazo walizipata.
Katika pambano hilo jopo la makocha walikuwa wakifuatilia kwa ukaribu burdani hio, makocha hao wakiongoza na kocha Hemedi Morocco walimchagua mchezaji wetu Helfini Salum kuwa ndiye mchezaji bora katika mchezo huo.
Usikose kufika Uwanja wa Amani siku ya Jumapili hii saa moja Usiku, kushuhudia burdani nyengine Kati ya Jang'ombe Boys FC na Shaba FC kutoka Kojani Pemba

Maoni