JANG'OMBE BOYS KUANZA LIGI KUU YA ZANZIBAR NA MAAFANDE WA KMKM



OUR ENGLISH READERS PLEASE SCROLL DOWN FOR THIS STORY


Msimu mpya wa ligi kuu Zanzibar  wa mwaka 2017/2018 unatarajiwa kuanza rasmi kesho kutwa Oktoba 3 panapo majaaliwa, ambapo Timu za Mafunzo na Jku zitakata Utepe majira ya saa nane adhuhuri.
Baada ya mchezo huo kutakuwa na mchezo mwengine mkali na wenye ushindani wa hali ya juu kati yetu Jang'ombe Boys na timu ya kikosi maalum cha kupambana na kuzuia magendo (KMKM), mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali sana na wa kusisimua, akithibitisha mbele ya wachezaji na washabiki juu ya ratiba ya mchezo huo baada ya mazoezi leo jioni tarehe 30 Septemba 2017, Katibu wa timu ya Jangombe Boys Abdallah Mahfoudh (Dallas) alisema kwamba mchezo wetu wa kwanza tutacheza na KMKM siku ya Jumanne ya tarehe 03 Oktoba saa 10 alasiri katika uwanja wa amani.
"Niseme kwamba tutakata utepe wa ligi na timu ya KMKM siku ya tarehe 03 Oktoba saa kumi jioni, katika uwanja wa Amani, ambapo mchezo huo utakuwa mgumu sana kutokana na historia yetu katika michezo iliyopita, hivyo Jumatatu tutafanya mazoezi yetu ya mwisho na niwaombe wachezaji waje kwa ajili ya kambi ya mechi, kwani baada ya mazoezi hatutarudi nyumbani tutakuwa kambini, ili kutengeneza umoja zaidi kwa mechi hio" Alisema Katibu Dallas.
Katibu wa Jang'ombe Boys Abdallah Mahfoudh aliye katikati
akitekeleza majukumu yake.

Katika hatua nyengine Katibu Dalas aliuambi mtandao huu kwamba, mchezo kati yetu na KMKM ni mgumu sana na ndio mchezo utakaotoa ramani halisi ya timu yetu na mwelekeo wake, kwa msimu huu unaonekana kuwa na ushindani zaidi, kutokana na timu zote kujikita kufanya usajili wa wachezaji wazuri.
"Kwa historia ya karibuni, timu yetu ndio kinara wa ubabe mbele ya KMKM kwa kuwa msimu uliopita wa ligi kuu ya Zanzibar (ZPL), tumeweza kukutana na KMKM mara mbili, katika mzunguko wa mwanzo, tuliwafunga KMKM kwa magoli 2-0 kwa magoli ya mshambuliaji wetu Khamis Mussa Makame (Rais) na lile la Abdulrahman Othman (Chinga) na mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi hio tulitoka sare ya 1-1 ambapo goli letu lilifungwa na Hafidh Barik (Fiy) " Alisema Katibu Dalas.
Ikumbukwe pia wakati wa dirisha la usajili KMKM walijaribu kutaka kumsajili mshambuliaji wetu khatari Khamis Mussa (Rais) pia walikuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji wetu Kinda Hafidh Barik (fiy) lakini waligonga mwamba, hivyo wa mantiki hiyo basi, ni dhahiri mchezo huo hautakuwa rahisi kwetu, kwani KMKM watakuja na dhamira ya kutaka kuweka historia sawa ya kufungwa na kushinda, sambamba na kuonyesha kwamba, ingawa waliwakosa wachezaji wetu  katika usajili wao lakini bado wana kikosi imara kinachoweza kupambana na timu yetu.
Nyote mnakaribishwa kuja kushuhudia mchezo huu mkali na wa kusisimua.
Mungu Ibariki Jang'ombe Boys - Amin


IN ENGLISH:

JANG'OMBE BOYS TO BEGIN WITH  KMKM SC.

The new season of Zanzibar Premier League (ZPL) of 2017/2018 is scheduled to be officially opened day after tomorrow 3rd October, where two brothers will meet on the football clash, this kick off will be between Mafunzo VS JKU who are both owned by the govenment of Zanzibar, this strip of the primier league will be cuted off at early at 14h00.

Later after this game there will be another pleasant and competitive game among us Jang'ombe Boys and Navy camp team  (KMKM), the game is expected to be very bright, tough, tactics and exciting, confirming before the players and fans during the training session this evening of 30 September 2017, Jangombe Boys Secretary, Mr. Abdallah Mahfoudh (Dallas) said, the first game will be kicked off with KMKM at 16h00 on Tuesday 3rd October this year at Amani Stadium.

"I would like to announce officially that, our team will be playing its first match league with the KMKM on 3rd October at 16:00 pm, in Amani Stadium, where the game seems to be very tough one due to our history in the last two games between us, therefore on Monday we will do our last exercise and I would like to advice  the players to come for a match camp on this day, because after the exercise we will not return home, because we are going to the camp for this match, this will help to create more unity for this match and moral building, "said Secretary Dallas.

 Also the Mr. Dalas told this network that the game between us and  KMKM is very difficult and is the game that will give us the real road map of our team and its direction, for this season it seems to be more competitive, because all teams arenot  reluctant to sign the most best  players for this new season.

"The latest history between two parties, show that we are super hero to them, since the last season of the Zanzibar Premier League (ZPL) we battled with  KMKM twice in premier league, the first round beat  KMKM with 2-0 goals, thanks to our striker Khamis Mussa Makame (Rais) and Abdulrahman Othman (Chinga) goals, and the second round of the league we drew 1-1, our goal was netted by Hafidh Barik (Fiy), "said Secretary Dalas.

It should also be noted that during the transfer window KMKM  hardly tried to sign our best striker  Khamis Mussa (Rais) also intend to sign our young striker Hafidh Barik (fiy) but they could not succeed, so obviously this game will not be easy for us , since KMKM will come up with a desire to keep the same history to us, in line with the fact that, although sfater missed our players for signing they want to show us that, still have a strong team that can compete our team.

On behalf of Jang’ombe Boys, you are all welcome to attend this  exciting game.

God Bless Jang'ombe Boys - Amen





Maoni