VILLA UNITED STRIVES TO BLOCK JANG'OMBE BOYS STORMS

The friendly match between us versus Villa United FC (Mpira Pesa) has ended tonight with the goalless result.

The match played at Amani Stadium was a type of entertainment due to both teams had young players with similar talent, but it was our team sides showed a great ability to hold the ball in both sessions.

Apparently seems that, the players took into account the training and reminder words from the head coach Mr. Said Kwimbi, which he told them on September 20, 2017, that he is not forcussing in winning this game but he need to see how to play the 3-5-2 system, where he wanted to see the support  of each other as a team in all 90 minutes of the game even if we will defeated.

"We're going in our friendly game with Villa United, what I want in this game, is to see how we are playing the 3-5-2 system, then if we need to well played in this system, we have to make sure we give support each other, if someone has a ball then there should be two to three people optional to be given a ball "said Coach Kwimbi.

Jang'ombe Boys Players warming up before match starts.

Since the players took into account the instructions and exercise perfectly, they were able to produce many opportunities to reach the Villa United goal, things force Villa decides to play on defensve style and Villa could prevent the storm from Jang'ombe Boys and make it possible for the game to survive to goalless (0-0).

The team will continue to exercise as usual tomorrow and Sunday night  will play another friend match with Shaba FC from Kojani Pemba, who are participating in the Zanzibar Premier League from Pemba side.

Come to enjoy the art of football in Zanzibar


TAFSIRI YA KISWAHILI:

VILLA UNITED WAJITAHIDI KUZUIA DHORUBA ZA JANG'OMBE BOYS

Mchezo wa kirafiki kati yetu na timu ya Villa United (Mpira pesa) umemalizika usiku huu kwa matokeo ya sare tasa.

Mchezo huo uliopigwa katika kiwanja cha Amani ulikuwa ni burdani ya aina yake kutokana na timu zote mbili kuwa na vijana wenye rika sawa na vipaji vinavyofanana, lakini timu yetu ilionyesha uwezo mkubwa wa kumiliki mpira vipindi vyote viwili.

Ilionekana dhahiri wachezaji waliyazingatia mafunzo na maneno ya kocha mkuu saidi Kwimbi aliyowaambia mnamo tarehe 20 Septemba 2017, kwamba anachokitafuta ni kuona jinsi gani wachezaji wataufanyia mazoezi mfumo wa 3-5-2, ambapo aliwataka kusaidia na wakati wote wa dakika 90 za mchezo hata kama wakifungwa.

"Tunakwenda katika mchezo wetu wa kirafiki na Villa United, ninachokitaka katika mchezo huu, ni kuona tunaweza kuutumia vyema mfumo wa 3-5-2, ili tuuweze mfumo huu ni lazima, tucheze kwa pamoja na tusadiane kila wakati, mtu anapokuwa na mpira basi kuwe kuna watu wawili mpaka watatu ambao wako huru kupokea pasi" alisema Kocha Kwimbi.

Kocha mkuu wa Jang'ombe Boys Said Kwimbi akitoa
maelekezo wakati wa mapumziko

Kwa kuwa wachezaji waliyazingatia maagizo ya mwalimu pamoja na kuyatumia mazoezi kikamilifu, walifanikiwa kuzalisha nafasi nyingi za kulifika lango la Villa United lakini kwa kuwa Villa waliamua kujikita zaidi na ulinzi waliweza kuzuia dhoruba na kuufanya mchezo uishie kwa matikeo ya bila kufungana (0-0).

 Timu itaendelea na mazoezi kama kawaida kesho alasiri na Jumapili saa moja usiku tutacheza mchezo mwengine na Shaba FC kutoka Kojani Pemba, ambao na wao wanashiriki ligi kuu ya Zanzibar Kanda ya Pemba.


Njooni muburudike.


Maoni