KILAHE' OF JANG' OMBE BOYS PACE SATISFY COACH KWIMBI.


Jang'ombe Boys fc's Right Defender  Hussein Said 'Kilahe' who last season of  Zanzibar Premier League 2016-17 often came in the pitch from bench, finally yesterday in a friendly match between Jang'ombe Boys versus Villa United become very brave and made his coach satisfied with his pace.

Speaking after the exercise this evening, Kwimbi said, 'Kilahe' did very good work in the last game with t Villa United FC, apart from his desperation and pace also Kwimbi wanted ‘Kilahe’ to multiply more efforts so as to do well and ultimately succeed in the football aspecially in this season.

'' Yesterday we have played our friendly game, we missed plenty of goals but we did well, and there are some players whom I cannot believe, they did a high-quality job, a  great performance ever, among them is ‘Kilahe’,  very good brother, you have shown a high level of performance in that game, though later you were overwhelmed by breath but to be honest you worked hard, so I advise you to put forth effort and practice personal exercise to keep yourself more comfortable with upcoming games" said coach Kwimbi.
Hussein Said 'Kilahe'

'Kilahe' appeared to have better position since the first minute of the game until the 70s minutes when he feels pain on his right side ribs and was subsequently evacuated into the Arahma hospital for investigation.

Kilahe highlighted the ability to overlap and his crosses went to targeted areas, and rarely were saved by the Villa's defenders and some of them caused the corners.
  


KASI YA 'KILAHE' WA JANG'OMBE BOYS YAMKOSHA KOCHA KWIMBI.

Mlinzi wa kulia wa Jang’ombe Boys FC Hussein Said maarufu ‘Kilahe’ ambaye msimu uliomalizika wa ligi kuu ya Zanzibar 2016-17 mara nyingi alikuwa akiingia akitokea kama mchezaji wa akiba, hatimae jana katika mchezo wa kirafiki kati ya Jang’ombe Boys na Villa United alimkosha Kocha wake mpya wa timu hiyo Said kwimbi.

Akizungumza baada ya mazoezi ya leo alimsifu ‘Kilahe’ kwa kazi nzuri aliyoifanya katika mchezo wa jana na timu ya Villa United, mbali ya kumsifia pia alimtaka kuzidisha juhudi Zaidi ili afanye vizuri na hatimae apate mafanikio katika soka.
Kocha mkuu, kocha msaidizi, daktari
Meneja vifaa wakifuatilia kwa Karibu
mazoezi ya timu.


‘’Jana tumecheza mchezo wetu wa kirafiki, tumekosa nafasi nyingi za magoli lakini kuna watu siwezi kuamini ‘Performance’ zao, walifanya kazi ya hali ya juu, Kilahe, nzuri sana ndugu yangu, umeonyesha uwezo wa hali ya juu katika mchezo wa jana, ingawa baadae ulizidiwa na pumzi lakini ulifanya kazi, hivyo nakunasihi engeza juhudi na ufanye mazoezi binafsi ili kujiweka sawa na vizuri Zaidi” Alisema Kocha Kwimbi.

‘Kilahe’  jana alianza kucheza katika kikosi cha mwanzo cha kocha 'Kwimbi' ambapo alionekana kuimudu vyema nafasi hio tangu dakika ya kwanza ya mchezo hadi dakika za 70 wakati alipoumia sehemu ya ubavu wa kulia na baadae kukimbizwa katika hospitali ya Arahma kwa uchunguzi.

Kilahe alionyesha umahiri wa kupanda na mipira na kupiga krosi nyingi zilizofika sehemu husika, mara chache krosi zake ziliokolewa na nyengine kuwababatiza mapeki wa timu ya Villa na kusababisha kona, mbali ya kocha Kwimbi, pia wadau a Jang'ombe Boys alivutiwa na 'Kilahe' katika mchezo huo, ambapo kila mara wadau waliokua jukwaani walimpongeza kwa kumpigia makofi kila ambapo alipokuwa akipanda na mpira.

'Kilahe' alifanyia uchunguzi hapo katika hospitali ya Alrahma nakutibiwa na baadae aliruhusiwa kurudi nyumbani akiwa amepona.


Maoni