JEE!WAJUWA KWAMBA CHINGA WA JANG'OMBE BOYS, BIBI HILLARY CLINTON WA MAREKANI NA RAIS KENYATTA WA KENYA WAMEZALIWA SIKU MOJA?

Ndio, mtandao huu umegunduwa kwamba siku ya leo Abrahman Othman Chinga hayuko peke yake katika kusherehekea siku hiyo bali kuna watu kadhaa ambao muda huu na wao wamo katika sherehe, dua na maandilizi mengineyo ya kuadhimisha siku hio.


Pichani aliyebebwa ni Chinga na Mbebaji ni Kocha Amasha

Mtndao huu umebaini kwamba leo ndio siku ambayo mama mzaa chema wa nyota huyu alipomleta duniani baada ya kupitia ukuta wake wa ‘facebook’ na kuona maandishi ynayoashiria uwepo wa siku hii, katika ukuta wake huo ameandika hivi:

"Namshukur mwenyezi mungu kwa kunijalia tena kufika siku yng ambayo nilokuja dunian sina budi kuwashukur wazazi wng wawili pamoja na familiya yng kwa kunilea vzr na kunipa matunzo mazur mpk Leo kufikia hivi nilivo pia na washukur rafik zng wote pamoja na majiran zng kwa upendo wao sina cha kuwalipa ila mungu atawalipa ila kama kuna mtu ambae nilomkosea naomba anisamehe na km yupo nilomkosea nimemsamehe ,Happy birthday to me" Aliandika Chinga

Ndipo mtandao huu ukagunduwa kwamba, siku ya leo pia ni siku ambayo wamezaliwa watu wengi mashuhuri na maarufu akiwemo Mke wa Rais wa Marekani na aliyekuwa mgombea wa uraus nchini Marekani katika uchaguzi uliomalizika bibi Hillary Clinton sambamba na Rais wa Kenya aliyepo madarakani Rais Uhuru Kenyatta pia wamo wanasiasa, wachezaji mpira, waimbaji, wanaharakati na wengine mbalimbali.

Kwa niaba ya timu nzima na wadau wote wa mtandao huu tunaungana na wote waliomtakia siku njema ya kuzaliwa.

"Happy Birthday to you"


Maoni