Kufutia kufungwa katika mchezo wa leo Makocha Jang'ombe Boys wamewataka wachezaji wao kutorudi nyuma.
Kocha mkuu wa Jang’ombe
Boys Said Kimbi amewataka wachezaji wake kuyakubali matokeo ya mchezo
uliomalizika kati ya timu yake dhidi ya timu ya Black Sailor, ambapo katika
mchezo huo Black Sailor wameweza kuifuga Jang’ombe Boys kwa goli moja
lililofungwa dakika ya 75.
Akizungumza na
mtandao huu baada ya kumalizika kwa dakika 90 za mchezo huo, kocha Kwimbi
amesema hakuna mabadiliko yatakayobadilika katika mchezo wa mpira wa miguu Zaidi
ya kushinda, kutoa sare na kushindwaa.
Kikosi cha Jang'ombe Boys
“Binafsi matokeo
nimeyakubali ingawa yanaumiza, hivyo nawasihi wachezaji wangu pia wayakubali
matokeo na wayapokee matokeo haya, kwani katika mpira a miguu zitakazobadilika
ni sharia tu, lakini matokeo ni haya haya, kushinda, kutoa sare na kufungwa,
umuhimu wa kuyakubali matokeo kama haya yatatusaidia kujipanga upya, kufanya ‘touch
up’ (masahihisho) na hatimae kufanya vyema katika michezo ijayo, ukizingatia
ligi bado ina safari ndefu.
“Hakuna jinsi ya
kuyageuza matokeo baada ya dakika 90 za mchezo, njia pekee ya kuyageuza matokeo
ni kushinda michezo ijayo, hakuna wa kumlaumu kwa sababu sote tulijitayarisha
ili tushinde lakini mpira ndio hivyo niseme ni mchezo wa ajabu ka sababu pale
unapotegemea matokeo fulani ndipo unapata yale matokeo usiyoyataraji” alimalizia
Kocha Kwimbi.
Kwa upande wa Kocha
msaidizi wa timu hiyo kocha Issa Othman (Amasha) amesema licha y kupoteza
mchezo wa leo bado anaamini kwamba bado timu yake ina kikosi bor Zaidikatika
msimu huu, hivyo hakuna cha kukatisha tamaa na kuitoa timu yake katika malengo
yake.
Akizungumz na mtandao
huu, kocha Amasha amewataka wachezaji wake kuyapokea matokeo haya ili iwe ndi
chachu y kufanya vyema mchezo unaofuata.
“Niseme kwamba hakuna
timu isiyofungwa, kila timu lazima ipitie matokeo kama haya, iwe mwanzoni au
mwishoni, hivyo anaelia mwanzo atacheka mwisho na anaecheka mwanzo atalia
mwisho, niwambie wachezaji kwamba ‘Hakuna kurudi nyuma’, matokeo kama
haya si mageni kwetu ikumbukwe hata ligi iliyomalizika tuliharibu michezo
mitano mfululizo lakini angalieni tulipojiuliza na tukarekebish na tukatengeza
ari zetu, nyinyi wenyewe mliona kilichotokea, naamini tukifanya kazi kwa pamoja tutacheza nane bora na hatimae kupata ubingwa” alisema Amasha.
Mchezo unaofuata
unategemewa kuchezwa tarehe 24/10/2017 dhidi ya Chuoni FC, mchezo amabo
utasukumwa katika dimba la uwanja wa Amani saa 10.00 alasiri.
Maoni
Chapisha Maoni