PIGA, UWA, GARAGAZA JANG’OMBE BOYS USHINDI DHIDI YA KILIMANI CITY KESHO LIGI KUU ZANZIBAR.




Kikosi cha Jang'ombe Boys 2017/2018


Viongozi, wachezaji na wadau wote wa Jang’ombe Boys FC inayonolewa na Kocha Saidi Kwimbi, wamesema mchezo wa kesho “Ama faimaa” lazima timu yao ishinde mchezo huo ili kuiweka timu katika mazingira ya matumaini na kurejesha matumaini kwa washabiki wake.

Na: Ali Mohammed.


VIONGOZI WATOA NENO ZITO:

Katibu wa Jang’ombe Boys Abdalla Mahfodh amesema kwamba kawaida ya timu hii huanza kwa kuharibu katika misimu yote ya ligi kunzia tangu madaraja ya chini, lakini utamaduni huu umeanza kuomekana kuwa haukubaliki tena katika timu hii, kwani ligi ya mara hii inaonekana haitatoa nafasi ya timu zilizoharibu mwanzoni kujirekebisha mwishoni.

“Imekuwa kama ndio utamaduni wetu kuharibu mechi kama tano hadi sita hivi halafu tena baada ya masahihisho ya makosa yetu huwa tunakaa sawa na kuanza kukusanya matokeo mazuri, lakini utamaduni huu haupendezi na wala hautoi dhamana katika ligi ya mwaka huu sioni kama kutakuwa na nafasi ya timu zilizoharibu mwanzoni kujisahihisha katikati au mwishoni, hivyo michezo mitatu inatosha sana na sasa hatutaki tena kuendelea na utamaduni huu na kesho Insha Allah ndio mwisho.

“Nasema hivi kwa sababu mwaka huu timu zinazoshiriki ligi ni timu 14 Pemba na 14 Unguja timu zinazoshuka Unguja ni 6 na Pemba ni sita, kwa hio kil timu imejipanga kuchukuwa alama mwanzoni, hivyo kama wewe umekosa mwanzo na mwenzako aliyekosa mwanzo haitakuwa rahisi kupata mwisho kwa menzio aliyekosa mwanzo kama wewe. Alisema Katibu Mahfoudh.

Kwa upande wa Rais wa timu Ali Othman Kibichwa, amesema kama ilivyolazima kufa kwa binadamu, basi ikiwa timu tunataka ikae katika mazingira ya kuonyesha kwamba tunatafuta nafasi, basi lazima timu itoke na alama zote tatu na si vyenginevyo.

“Kesho kama tunataka kuiweka timu yetu katika mazingira ya kutafuta nafasi katika ligi, basi ushindi ni muhimu na lazima 'kama ilivyokufa na binadamu', matokeo yeyote kinyume na ushindi ni kusema tunaendelea kupoteza nafasi au tunajiweka katika mazingira magumu katika kutafuta nafasi.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika vizuri, tayari timu imeingia kambini ikiwa na wachezaji 29 na wachezaji wana ari na mchezo na wametuahidi ushindi sisi viongozi na washabiki na wewe ndugu mwandishi ukiwa shahidi. Alisema Ali Othman.

MAKOCHA WANG’AKA:

Kama tujuavyo Jang’ombe Boys FC mwaka huu imesajili kocha Said Kwimbi ambaye kabla aliwahi kufundisha timu ya Kilimani City, hivyo kuna mengi yanzugumza na Kilimani City, kuna shutuma za kwamba eti hata wachezaji waliosainiwa na Jang’ombe Boys wamejiunga hapa kwa ushawishi wa Kwimbi, jambo ambalo kwimbi mwenyewe amelipinga vikali sana.

“Kesho tunacheza mchezo wetu wan ne ambao ni rahisi lakini ni mgumu na nitawaeleza kwa nini ni mgumu, kuna shutma dhidi yangu kwamba eti hawa mabwana, Pichori na Fini kwamba nimewaleta mimi katika timu, kitendo ambacho mimi sikikubali, kwa sababu Issa anajuwa kwamba mimi nilishasema kwamba kwa kipindi hichi sitaki kujihusisha na ukufunzi wa mpira, lakini Issa ndio akaniomba nije tusaidiane baada ya yeye kupata fununu za kocha Maha kujiunga na Miembeni City, lakini kauli yangu hii haikubaliki ndani ya Kilimani City.

“Hizi timu zina visasi vyao tangu huko chini, hivyo visasi hivi vitaendelea na kesho ndio siku yenyewe ya visasi kuendelea, ila mpia dakika 90 lakini timu yangu naiamini na natosheka kuamini kwamba kesho ndio ligi kiupande wetu Insha Allah tutaianza kwa matokeo yatakayotuonda hapa tulipo na kutusogeza kuelekea kule tunakokutaka ambako ndiko mahali timu hii inastahiki kuweka maskani kimsimamo. Alisema Kwimbi.

Nae Kocha Msaidizi Issa Othman (Amasha) amesema, anajuwa uhasama uliopo baina ya timu hizi, anajuwa hasira walizo nazo kilimani City baada ya kuwachukuwa wachezaji wake wawili katika usiku wa mwisho a dirisha la usajili.

“Najuwa uhasama wa kimchezo baina yetu na Kilimani City, najuwa jinsi gani tulivyowavuruga tulipowasajili Helfeni na Suleiman (Pichori), hasa kitendo cha usiku wa mwisho wa kufungwa kwa dirisha la usajili, ile ilikuw bakora kubwa na mbaya sana, hivyo mchezo ni mgumu lakini ushindi mechi hii ni lazima” Alisema Amasha.

KAPTENI NAE AKAZIA:

Mbali ya viongozi hao waliotangulia kuwahakikishia wadau wa Jang’ombe Boys kwamba timu itafurahisha katika mchezo wa kesho, nae Kepteni wa timu Ibrahim Mohammed (Sangula) hakuwa mbali na mwandishi wa mtandao huu aliyekuepo uwanja wa mazoezi wa timu hiyo ili kuzungumzia mchezo huu nae alieleza haya:

“Baada ya kupokea ahadi nyingi kutoka kwa wadau wetu, na mimi nashawishika na kulazimika kusema kwamba, wachezaji wenzangu wote tumeshainingia katika mchezo huu na iliyobakia baada ya wiki kadhaa za kusuwa suwa.

“Nadhani pale pembeni unaona shehena ya mapegi, yale ni mabegi ya wachezaji sote 29 tuliosajiliwa na timu hii kwa msimu huu, hivyo kuna tafauti kubwa sana ukilinganisha na michezo mitatu iliyopita, michezo iliyopita hatukuwa tukiingia kambini sote lakini kuanzia sasa tumeshikamana kwa pamoja ili kuleta ushindi katika kila mechi kuanzia hii ya kesho.

“Hivyo nawambia City majirani, ndugu zetu wajitayarishe na mateso ya kesho panapo majaaliwa, tunajuwa tumejiandaa lakini mtiti huu kesho hakuna kuni ya nyongeza, tunapanga magogo ya uhakika hata “Bulldozer” hlitaweza kuondoa magogo hayo, na jambo zuri hata makocha wetu kwa mchezo huu leo tunondoka nao kuingia kambi, hii itasaidia kumaliza mchezo mapema sana Insha Allah. Alimaliza Sangula.

KUMBUKUMBU ZA MICHEZO ILIYOPITA:

Timu hizi kwa kumbukumbu za michezo minne ya karibuni yanaibeba Jang’ombe Boys FC, ambapo mchezo wa kwanza katika mine hiyo Jang’ombe Boys walishinda 2-1 ka magoli ya Edo na Rais, mchezo wa pili tukatoka sare ya goli 3-3 magoli ya Jang’ombe Boys yalifungwa na Chinga, Beka Raul na Eddo, mchezo wa tatu tukwafunga kilimani City 1-0 kwa goli la Kilahe na mchezo wa mwisho katika uwanja wa fuoni tukitumia kikosi ‘B’ City walishinda 2-1.

Kwa niaba ya wafanyakazi wa mtandao huu, tunaiombea timu yetu Jang’ombe Boys FC ushindi wa kishindo katika mchezo huo mkali na wa kusisimua dhidi ya Kilimani City.

AMIN



Maoni