RATIBA YETU YA KESHO J. BOYS KUWEKA REKODI MPYA



Kesho tutashuka tena Kiwanjani kucheza mchezo wetu mwengine muhimu katika michezo ya ligi kuu Zanzibar, mchezo huu ni watatu kwetu, kutokana na uzuri wa wachezaji wetu mmoja mmoja nalazimika kusema michezo yetu miwili ya mwanzo tumepoteza, ingawa kimahesabu ya mpira tumepoteza mchezo mmoja na kwenda sare mmoja.

Mchezo wetu wa kwanza na KMKM tulitoka sare ya goli 1-1 mfungaji wa goli letu alikuwa ni Khamis Mussa (Rais) na mchezo wetu wa pili tukafungwa na Black Sailors FC goli 1-0, ambao kwa historia timu hii ni wapinzani wetu.

Kesho vile vile tufahamu tunacheza mchezo mmoja mgumu sana kwa timu yetu, kwa sababu timu yetu haina kumbukumbu nzuri na timu hii, hakuna rekodi ya kuwafunga Chuoni, lakini katika maisha rikodi huvunjwa kitu pekee kisichofunjika ni historia kwa sababu ni kitu ambacho kimeshafanyika na hakirudiwi tena kufanyika na hata kikifanyika huwa ni kitu kingine kipya.

Hivyo mchezo wa kesho wachezaji wamehamasika na wameahidi kuandika rikodi mpya, kuondoa uteja kwa Chuoni na uteja hapa si kutoa suluhu, hapana, zipo kumbukumbu zinazoonyesha tumeshatoa suluhu michezo kadhaa, lakini kesho wachezaji wameahidi kutuzawadia ushindi wetu wa kwanza ingawa wanaelewa kwamba Chuoni nao pia wamejiandaa.

Kimachotakiwa kwetu wadau, washabiki, wanachama na wapenzi kuiombea kheri timu yetu na kufika Kiwanjani kwa wingi kuishangilia timu sambamba na kupokea zawadi ya ushindi wa mwanzo kwa kuwafunga Chuoni FC sambamba na kupokea ushindi wa kwanza kwa timu yetu tangu ligi ianze.

Kila la kheri Jang'ombe Boys.


Maoni