‘SANGULA’ ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA WATU MAARUFU NA MSHUHURI DUNIANI.

Wakati Kapteni wa timu yetu Ibrahim Mohammed ‘Sangula’ akiwa katika shukrani za kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia kutimiza umri alionao kwa salama na uzima wa afya, mtandao huu umegunduwa kwamba siku ya leo Ibrahim hayuko peke yake katika kusherehekea siku hiyo bali kuna watu kadhaa ambao muda huu na wao wamo katika sherehe, dua na maandilizi mengineyo ya kuadhimisha siku hio.




Mtndao huu umebaini kwamba leo ndio siku ambayo mama mzaa chema wa nyota huyu alipomleta duniani baada ya kupitia ukuta wake wa ‘facebook’ na kuona maandishi ynayoashiria uwepo wa siku hii, katika ukuta wake huo ameandika hivi:

"Nashukuru mungu kwa kunijalia kunifikisha tena siku yangu ya leo ya kuzaliwa me hakuna. mwenye uwezo huo isipokuwa ni yeye pekee pia na nawshukuru wazazi wangu kwa kulea vizuri na kunitunza pia naishukuru familia yangu kwa kuishi pamoja kwa mapenzi pia nawashukuru marafiki zangu wote na maadui zangu kwa siku ya leo kuzaliwa kwangu nawapenda sana happy birthday to me" aliandika Sangula.

Ndipo mtandao huu ukagunduwa kwamba, siku ya leo pia ni siku ambayo wamezaliwa watu wengi mashuhuri na maarufu akiwemo muimbaji SHAGGY kutoka JAMAICA  pia wamo wanasiasa, wachezaji mpira, waimbaji, wanaharakati na wengine mbalimbali.

Wanasiasa:
John Shadegg, Gavana wa zamani wa jimbo la Arizona - Marekani
Bill Owen, Gavana wa Colorado - Marekani
Seif Sharrif Hamad, Katibu Mkuu a CUF - Tanzania.
Patrick  Mc hendry, Congress Califonia.
Harry Moniba, Makamo wa Rais wa Zamani wa Liberia.
Joaquim Cissano, Rais mstaafu wa Zambia

Makocha:
Arsene Wenger, Arsenal FC
Brad Stevens, Reading, Sligo Rovers, Nothern Ireland, Fulham, Wycombe Wanderers nk

Wachezaji Mpira:
Michael Salgado, Mchezaji wa zamani wa hispania
Otis Smith, Mchezaji a zamani wa marekni
Andre palop mchezaji wa zamani wa hispania.
Ichiro Suzuki, mchezaji wa zamani wa Japan.
Chaswe Nsofwa, mchezaji wa zamani wa Zambia
Doni, Mchezaji wa zamani wa Brazil.

Orodha hio fupi ni miongoni mwa watu mashuhuri, lakini orodha hio si ukamilifu wa watu mashuhuri waliozaliwa siku ya leo sambamba na nyota wetu Ibrahim Mohammed (Sangula), bali hao ni wachache sana, miongoni mwao wameshatangulia mbele ya haki.

Kwa niaba ya timu nzima na wadau wote wa mtandao huu tunaungana na wote waliomtakia siku njema ya kuzaliwa.

"Happy Birthday to you"

















Maoni