HABARI ZA HIVI PUNDE: SANGULA NA RAIS WAMECHAGULIWA KATIKA TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba, kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) , Hemed Suleiman (Morocco)  jioni hii tayari  ametangaza majina ya wachezaji watakaounda kikosi cha timu hiyo.



Katika kikosi hicho Kocha 'Morocco' amechagua wachezaji wawili wa timu yetu Jang'ombe Boys kuunda Zanzibar Heroes, wachezaji hao ni beki kisiki wa kati na kepteni wetu Ibrahim Mohammed (Sangula) na mshambuliaji wetu khatari Khamis Mussa (Rais) .

Kujuwa kikosi kamili cha Zanzibar Heroes, mtandao huu utakuekea majina yote ya wachezaji waliochaguliwa na timu wanazotoka.

Usiende mbali, baki nasi 24x7.

Maoni