NANI MKALI KATI YA RAIS NA HILIKA?

Wote ni washambuliaji tegemeo waliochaguliwa na kocha mkuu wa  timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kocha Hemed Suelima (Morocco).

Fika jumapili tarehe 12/11/2017 saa 8 mchana katika Kiwanja cha Amani ushuhudie wakali hawa wawili wanaochezea timu tofauti yaani khamis Mussa 'Rais' wa Jang'ombe Boys na Ibrahim Hamad Hilika 'Mbape' wa Zimamoto.

Siku hiyo mbali ya kuonyesha ukali kwa washabiki wao bali pia wataonyesha kwa kocha wao nani anamzidi mwenzako kwa ukali wa kupachika mabao.


Maoni