Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amekubali maombi ya kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroko ya kutaka amualike Rais wa chama cha soka cha Afrika Ahmad Ahmad kuja Zanzibar kujionea hali ya mpira wa Zanzibar.
Rais Shein ameyakubali maombi hayo mbele ya Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zamzibar Heroes) wakati wa taarab maalum na ghafla ya utoaji wa Zawadi kwa Zanzibar Zamzibar Heroes na amesema atamualika Rais huyo kuja Zanzibar kujionea soka la Zanzibar na pia kuweza kumshawishi kuweza kuirejeshea Zanzibar uwanachama wa CAF.
Maombi hayo ya Kocha Morocco yana lengo la kufungua mazungumzo ya namna gani Zanzibara itakuwa mwanachama wa CAF, baada kufutiwa uanachama wake uliodumu kwa miezi minne pekee tangu Zanzibar ilipopata uanachama rasmi wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC, ni kuwa Rais wa CAF, Ahmad Ahmad ndiye aliyeamuwa kufuta uanachama wa CAF wa Zamzibar kwa kusema kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na haikutakiwa kupewa uanachama huo ambapo ilikuwa mwanachana wa 55 kutokana na baadhi ya mambo kukiukwa.
"Walipewa uanachama bila kufuata taratibu zote, Caf haiwezi kukubali kuwa na wanachama wawili ndani ya nchi moja.
"Maana ya taifa inakuja kutokana na kutambulika na Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa (UN)," alisema rais huyo.
Katika hatua nyengine Dk. Shein amesema yuko tayari hata KUMUALIKA rais wa FIFA kuja Zanzibar.
Maoni
Chapisha Maoni