FA ZANZIBAR TUEKEENI KIKOSI BORA CHA MWAKA CHA LIGI YA ZANZIBAR 2017

Nchi zote duniani zenye ligi za mpira wa miguu (Premier leagues) zimeshatangaza vikosi vyao vya mwaka 2017, na hata zilizokuwa hazijatangaza basi wako hatua za mwisho kufanya hivyo.

Yaani kuchagua wachezaji walionyesha kwanubora katika kila nafasi na hatimae kutaja kikosi bora chanye wachezaji kutoka vilabu mbali mbali vya ligi hizo waliocheza vyema.

Hii Haina gharama ni kufanya uchaguzi wa wachezaji na baadae kuwatangazia waandishi wa habari na waandishi na wao hutangaza katika vituo vyao wanavyotumikia yakiwemo magazeti, Televisheni, Redio n.k.

Hakuna zawadi itolewayo kwa wachezaji hao, lakini inasaidia sanasana katika kukuza viwango vya wachezaji, inasaidia vilabu kuimarika vikosi vyao na hata kuwasogeza washabiki karibu na ligi yao sambamba na kufanya ushawishi wa washabiki wapya.

FA Zanzibar tutoleeni kikosi cha 2017 kama mlishaandaa kama hamjaandaa tunaomba mtuandalie huu muda ulobakia, hivi ni vimambo vidogo lakini vinanogesha ligi na kuleta hamasa kwa wachezaji na washabiki wa mpira wa miguu.

Ali Mohammed
Zanzibar

Maoni