HATIMAE 'BALII' ARUDI MIEMBENI CITY NA 'FIY' AJIUNGA NA ZIMAMOTO

Katika tetesi za uhamisho wa wachezaji katika timu za ligi ya Zanzibar zilizokuwa zimetawala vinywani mwa washabiki wa mpira wa miguu Zanzibar hazikuyaacha majina mawili haya salam, yaani Ali Humudi Badru (Balii) na Hafidha Barik (Fiy).

Ni hakika usajili huanza na uvumi na uvumi juu ya wachezaji hao umegeuka kuwa ukweli baada ya timu yetu kupokea fomu za uhamisho kutoka vilabu vya Miembeni City ambapo Ali Humudi badru alikohamia sambamba na klabu ya Zimamoto ambayo mshambuliaji Hafidh Barik (fiy) alikohamia.

                              Ali Humud Badru (Balii)                        Hafidh Barik (Fiy)

Ikumbukwe katika mchezo wa mpira si mara nyingi mchezaji kubakia na timu fulani kwa muda mrefu, ni wachezaji wachache tu ambao wenye uzalendo na uananchi na kuamini kwamba maendeleo ya mpira wanaweza kuyapata popote hata wasipohama na kuhamia timu nyengine.

Tunakiri kwamba tumeondokewa na wachezaji bora na wenye vipaji, lakisi kama Jang'ombe Boys hatuna kinyongo wala huzuni kwa hilo, kwa sababu tunaamini kwamba timu yetu ni kisima cha vipaji, hivyo kuondoka kwa mchezaji mmoja ndio kamati yetu ya usajili inabaini kipaji kipya na kukileta katika timu yetu na hatimae kuwa kipenzi cha timu yetu kama walivyokuwa waliopita na kuondoka, na hili tumelithibitisha mara nyingi.

Hivyo tunawatakia kila la kheri wachezaji hawa na wale ambao wako katika mazungumzo ya kuhamia vilabu mbali mbali, waende huko wakafanye vizuri kama tulipokuwa nao na hatimae waende mbele zaidi ya hapo walipokwenda.

Na kwa washabiki wetu tunapenda kuwatoa shaka vifaa vipya vipo tayari vinajiunga na timu yetu baadhi yao tuliwaonyesha katika mchezo wetu na Gulioni, na vyengine mtaviona wiki hizi mbili, na hatimae mtakuja kukiri ligi itakaporudi baada ya kumalizika Kombe la Mapinduzi hapo Januari 2018.


Maoni