JANG'OMBE BOYS KUFANYA 'TOUR' MAALUM, DUA YA KUUTAKIA KHERI MWAKA MPYA WA 2018 NA MAMBO MENGINE MAZURI
Timu ya Jang'ombe Boys imeandaa mambo mbali katika kipindi hichi ambacho ligi imesimama kwa kupisha kombe la Mapinduzi, miongoni mwa mambo hayo ni kuitangaza timu kwa kucheza michezo ya kirafiki na vilabu mbali mbali vilivyo nje ya mji wa Zanzibar, ambapo kuanzia leo Alhamis tutacheza na timu ya kijiji cha Maungani inayoitwa Maungani FC hapo hapo katika kiwanja cha Maungani FC.
Ratiba nyengine itathibitishwa baada ya mchezo huo wa Maungani ambapo unataraijiwa kuwa mchezo na timu ya Kinyasini kaskazini Unguja ambapo pia ina mpango siku hio timu ilale huko huko Kinyasini ili siku inayofuata icheze na timu nyengine katika mkoa huo wa kaskazini.
Kwa upande wa Friends of J. Boys wao wameandaa dua maalum ya kuliombea taifa kuwa na hali ya amani na usalama ili Mwenyezi Mungu atulindie nchi yetu na majanga mbali mbali yale yaliyo ya 'Qadari' na yale ambayo husababishwa na viumbe, dua hio itasomwa katika msikiti wa Jeshi kwa wanaume na wanawake itasomwa katika chuo cha Mwalim Khiyari.
Friends of Boys, pia wameandaa tunzo maalum kwa wachezaji wao, kutakuwa na tunzo za mchezaji bora wa mwaka, mfungaji bora wa mwaka, mchezaji mdogo katika kikosi kwa mwaka, mshabiki bora wa kiume na kike na zawadi nyenginezo, zawadi zinazohusu wachezaji pia watahusishwa hata wale wachezaji ambao wamehama timu, endapo wataangukia kuwa miongoni mwa waliopitishwa na jopo la waamuzi basi wataalikwa kuja kuchukuwa zawadi zao.
Pia kutakuwa na safari maalum ya kuwatembelea watoto mayatima hapo katika nyumba ya mayatima Mpendae sambamba na kuwanasihi ndugu zetu waliopo katika nyumba ya Soba ( Sobber House) kuendelea na uvumilivu wa kuacha kutumia madawa ya kulevya.
Mgeni rasmi wa shughuli zetu zote hizi tunatarajia atakuwa Mh. Mkuu wa Mkoa wetu wa Mjini Magharibi, shughuli hii itafanyika siku ya Jumapiti ya tarehe 31/12/2017.
Mnaombwa kuiunga mkono timu yenu, ili mipango yote ikamilike kama ilivyopangwa

Maoni
Chapisha Maoni