HICHI HAPA KIKOSI CHA ZANZIBAR HEROES KITAKACHOIGARAGAZA KENYA

Ni siku nyengine tena ya mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup 2017 huko Kenya ambapo ratiba ya kesho inaonyesha kutakuwa na michezo miwili ya kundi A, mchezo wa mwanzo saa 8 za adhuhuri utakuwa kati ya Rwanda na Tanzania Bara, ambazo timu mbili zimeshagaragazwa na Zanzibar Heroes, Rwanda walifungwa 3-1 na Tanzania bara walifungwa 2-1.

Mchezo wa pili ni kati ya wenyeji Kenya na Zanzibar, mchezo utapigwa majira ya saa 10 alaasiri, kuthibitisha uwepo wa mchezo huo kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) tayari aeachia kikosi kitakachopambana na Kenya, kikosi kiko hivi:
Kikosi cha Zanzibar Heroes 2017

Kikosi cha Kwanza:
Mohammed Abrahman (Wawesha)
Ibrahim Mohammed (Sangula)
Haji Mwinyi
Abdullah Kheri (Sebo)
Issa Haidar Dau (Mwalala)
Abdul Aziz Makame (Abui)
Mohd Issa (Banka)
Mudathir Yahya
Ibrahim Hamad Hilika
Feisal Salum (Fei toto)
Suleiman Kassim (Seleembe) - Nahodha wa Kikosi.

Wachezaji wa Akiba:
Ahmed Ali 'Salula'
Ibrahim Abdallah
Adeyum Saleh
Abdulla Haji (Ninja)
Seif Rashid (Karihe)
Kassim Suleiman
Khamis Mussa (Rais)
Amour Suleiman (Pwina)
Hamad Mshamata
Abdul Swamad Kassim (Hazgut).

Dua zetu muhimu ili Zanzibar Heroes Ishinde.

Maoni