Baada ya Kamati ya Kombe la Mapinduzi kutoa ratiba ya Kombe la Mapinduzi,kumekuwa na mjadala mrefu juu ya uwepo wa mchezo wa kirafiki wa kufunga Bonanza lililoandandaliwa na Kampuni ya Rafiki Network, ambapo mchezo huo unatazamiwa kuchezwa tarehe 31/12/2017 saa mbili na nusu usiku (02.30)
Kwa mujibu wa ratiba ya kombe la Mapinduzi inayoenea mitandaoni ni kwamba siku hio ya tarehe 31/12/2017 kutakuwa na michezo michezo miwili ya kundi B, mchezo mmoja utachezwa saa 10.30 ambao ni kati ya Zimamoto na JKU na mchezo wa pili utachezwa saa 2.30 usiku ambao utachezwa kati ya Mlandege na Taifa ya Jangombe, ambapo kwa mujibu wa Rafiki Network, Jangombe Boys, Taifa ya Jangombe ni kwamba siku hiyo kutakuwa na mchezo wa funga mwaka kati ya Jangombe Boys na Taifa ya Jangombe saa 2.30 usiku.
Mchezo huo ulikwishapata baraka zote, kuanzia uongozi wa Uwanja wa Amani, ZFA, Jang'ombe Boys, Taifa ya Jang'ombe, na mazungumzo ya mchezo huo yamekuwa yakifanywa kwa pamoja katika ya Waandaaji (Rafiki Network), uongozi wa Jang'ombe Boys na Taifa ya Jang'ombe.
Mchezo huo ni mkubwa kwani kwa mujibu wa waandaaji, Rais wa Zanzibar ameshathibitisha kuwa mgeni rasmi wa mchezo huo akiambatana na mawaziri wa serikali yake, wawakilishi na viongozi wa ngazi mabalimbali.
Tiketi za mchezo huo zimeshauzwa na kwa taarifa kwamba zile za VIP zimemalizika, zile za sh.3000/- zinakaribia kumalizika na zile za 5,000/- watu wanaendelea kumiminika kuzinunua, na hapo ndipo palipojengeka khofu kwa wale waliokwisha kujinunulia tiketi hizo.
Mtandao huu unapenda kuwatoa khofu wadau wote wa mchezo huu, hakuna haki ya mtu itakayopotea kwani mchezo huu bado upo kama ulivyopangwa, inaonekana hakukuwa na mawasiliano baina ya kamati ya mapinduzi na uongozi wa uwanja, kitu ambacho kamati ikaamuwa kuitumia siku na wakati huo kupanga mchezo huo na timu hiyo ambayo ndio mshiriki mwenza wa mchezo huo wa Bonanza la Rafiki Network.
Timu yetu kupitia Afisa wetu Ali Mohammed ameshawasiliana na watendaji wa Rafiki Network na wao wamepatwa na mshangao kuona ratiba hio kwa michezo yote miwili, kwa sababu za kiintelijensia na ujio wa rais wa Zanzibar siku hiyo hakukutakiwa kuchezwa mchezo hata mmoja siku hio kuanzia jioni hadi usiku.
"Sisi ratiba yetu iko palepale na ilishathibitishwa na uongozi wa uwanja, sasa kinachoonekana kamati ya Mapinduzi haina taarifa rasmi za mechi hio, lakini si tatizo tunalifatilia ili kuweka sawa hali hii na niseme kwamba mchezo wetu uko palepale, na wale walionunua tiketi wasiwe na shaka, na kwa wale waliokuwa hawajanunu tiketi wanunuwe wasije wakakosa burdani siku hiyo" alisema afisa wa Rafiki Network.
Hivyo mnaombwa nyote wadau wa mchezo huo, muondoe khofu mchezo upo kama kawaida, na ikiwa kuna mtu yeyote anaekebehi juu ya kutokuepo kwa mchezo huo, basi huyo apuuzwe tu, kwani inaoneka hajui alitendalo na wala hajui lililopo, kwani huu ni mchezo wa utatu baina ya waandaaji na vilabu vyote viwili, yaani Jang'ombe Boys na Taifa ya Jang'ombe, na hakuna timu iliyotenzwa nguvu kucheza mchezo huu, tulikubalina kwa pamoja hivyo hakuna sababu ya kuamini kwambaeti kuna timu imehairi kucheza au kukimbia pambano ni mambo madogo tu yakurekebishwa na hatimae yatarekebishika.
Tutawajulisha zaidi baada ya Rafiki Network kulieka sawa suala hili
Kampuni inayoandaa mechi ya Jang'ombe Boys vs Taifa ya Jang'ombe 31/12/2017
saa mbili na nusu 02.30 usiku

Ratiba ya Kombe la Mapinduzi 2017/18

Maoni
Chapisha Maoni