KOCHA MOROCCO AONGEZA DAMU CHANGA KATIKA KIKOSI CHA 'ZANZIBAR HEROES' KILICHOKWENDA PEMBA

Zamu ya wakaazi wa Pemba kuwaona mashujaa wa Zanzibar 'Zanzibar Heroes' ndio hivyo imefika, tayari hio ipo katikati ya bahari muda huu kuelekea Pemba, timu hiyo iliyo chini ya Kocha wake Hemed Suleiman (Morocco) imeondoka asubuhi hii kuelekea Pemba ambapo huko itacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kombaini ya Pemba.

Helfini Salim (fini) wa katikati mwenye shati nyeupe

Maamuzi hayo ya timu ya Taifa ya Zanzibar kwenda kisiwani Pemba ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk. Ali Mohammed Shein, agizo ambalo alilitoa siku ya tarehe 23 Disemba mwaka huu wakati wa tafrija maalum iliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani, ambapo Dk. Shein aliwazawadia wachezaji hao wa ZH na viongozi wao kiasi cha shilingi milioni 3 kila mmoja na kiwanja kimoja kimoja cha kujengea nyumba.

Katika hatua nyengine, Kocha Mkuu wa timu hiyo amewaita wachezaji wawili wapya katika kikosi hicho ikiwa pia ni kufuata agizo la Dk. Shein kwamba timu hiyo isivunjwe bali iengezewe nguvu ili idumu kwa muda mrefu.

Wachezaji hao walioitwa ni mlinzi wa kati Ali Humud Badru (Balii) ambaye alikuwa akicheza timu ya Jang'ombe Boys, ambapo jana amehama timu hio na kuhamia Miembeni City na mwengine ni Kiungo mshambuliaji wa Jang'ombe Boys Helfini Salum ambaye ana miaka 18,  hivyo wachezaji hawa wameungana na wenzao walioiwakilisha Zanzibar katika mashindano ya CECAFA.

Maoni