KAMPUNI YA 'RAFIKI NETWORK' YAWAALIKA ZANZIBAR HEROES KATIKA MECHI KATI YA JANG'OMBE BOYS NA GULIONI








Kampuni inayojihusisha na kuandaa matamasha ya michezo mbali mbali iitwayo http://rafikinetwork.net/ ambayo hivi sasa iko katika maandalizi yake ya Bonanza la kufungia mwaka, imeandaa mchezo maalum  Kati ya Jang'ombe Boys na Gulioni City.

Katika mchezo huo msafara mzima wa Zanzibar Heroes umealikwa, hivyo nikusema mashujaa wetu wa Zanzibar Heroes watakuepo kiwanjani Amani siku ya tarehe 25/12/2017 saa 2.30 usiku kuangalia mpambano huo ambao utakuwa na Kombe uwanjani, yaani mshindi atapatiwa kikombe na fedha taslim ambazo bado hazijaelezwa na waandaaji ni kiasi gani.


Kikosi cha Jang'ombe Boys 2017

Ikumbukwe awali mchezo huu ulipangwa kuchezwa 31/12/2017 kati ya Jang'ombe Boys dhidi ya Taifa ya Jang'ombe,lakini kutokana na sababu za Taifa kuwemo katika Kombe la Mapinduzi na changamoto nyenginezo zimepelekea mchezo huo kutokuwepo, na Rafiki Network kwa kuwa ni watu wa michezo na lengo lao ni kuwaita watu katika michezo ndipo wakarudi na wazo hili la kuchezwa mchezo huu.


Rafiki Network katika mipango yao walipanga mshindi kati Jang'ombe Boys na Taifa, licha ya zawadi kwa mshindi na mshindwa lakini walikusudia kutangaza baada ya mchezo huo, mshindi angepata nafasi ya kucheza na timu ambayo ingetoka nje ya Tanzania aidha kutoka Ulaya au Afrika Magharibi.

Kwa kuonyesha kwamba mchezo huo ni maalum basi fursa hio inatolewa pia kwa timu hizi, timu itakayoibuka bingwa katika mchezo huu mbali ya Zawadi ya ubingwa basi atapata fursa ya kujipima nguvu na timu moja wapo kutoka Ulaya au Afrika Magharibi ambayo itatangazwa hapo baada ya kufikia makubaliano na klabu itakayokuwa tayari kuja Zanzibar baada ya kumaliza ligi za nchi zao.
Kikosi cha Gulioni

Hivyo washabiki wa Zanzibar Heroes, washabiki wa Gulioni City, washabiki wa Jang'ombe Boys na wapenda mpira wote njooni siku hio mushuhudie mambo mazuri yaliyoandaliwa na waandaaji mahiri wa matamasha ya michezo Zanzibar Rafiki Network, kwani wameahidi mbali ya mchezo huo wa mpira wa miguu lakini kutakuwa na burdani mbalimbali ambazo hazijawahi kuonekana katika uwanja wa Aman.

Mgeni Rasmi huenda akawa Dk. Ali Mohammed Shein au kiongozi mwengine yeyote wa juu wa Zanzibar au Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, nani atakuwa mgeni rasmi, mtajulishwa baadae. 

Ahsanteni.

Maoni