Hatimae Zanzibar Herous imepata ushindi katika mchezo wake wa mwanzo katika mashindano ya CECAFA Senior cup, ambapo imeibuka na ushindi wa magoli matatu kwa moja dhidi ya Rwanda.
Kikosi cha Zanzibar Heroes kilichoifunga
Rwanda 3-1
Baada ya mchezo huo inasemekana mlinzi Ibrahim Mohammed (Sangula) ambaye ni Nahodha wa Jang'ombe Boys ambaye alicheza katika kikosi hicho cha Zanzibar Herous kilichoifunga Rwamda alilia sana na hadi kusababisha kuondolewa Kiwanjani akiwa amebebwa.
Mtandao huu ulifanya mawasiliano na Nahodha Huyo kwa njia ya simu alisema hakuna likubwa kilichomfanya amwage chozi bali ni uzalendo na kuumwa na nchi yake.
"Nikweli taarifa hizo ni sahihi nimelia sana, si jambo jengine lililoniliza bali ni uzalendo kuona mimi na wenzamgu tumelitetea taifa letu na tumewaletea kile Wazanzibari walichokitegemea kutoka kwetu.
"Jengime Siamini kama iko siku mimi nitakuwa mchezaji na nitatetea taifa langu
Kupitia mpira wa miguu, pia nimelia kwa furaha kwa mara yangu ya kwanza nacheza mashindo makubwa, tena nikiwa ugenini nikiwa nacheza kwa kujiamini bila kujali kwamba niko ugenini.
"Hivyo niwaombe washabiki wetu, Wazanzibari, viongozi wetu na wadau wote wa michezo tuungane kwa pamoja kuiombea timu yetu ushindi katika michezo inayofuata na hatimae tupate ubingwa wa mashindano hayo kwa mara ya pili" Alimalizia Sangula
Maoni
Chapisha Maoni