Wengi walizoea kumuona Nahodha wa timu yetu Ibrahim Mohammed (Sangula) akicheza beki ya katikati, na kiukweli Imani za Wazanzibari wote walimuamini na kuamini kwamba uhodari wake unakuja tu pale anapocheza nafasi hio na si vyenginevyo.
Nahodha wa Jang'ombe Boys na mlinzi wa 'Zanzibar Heroes' Ibrahim Mohammed 'Sangula'
Lakini hali ikawa tofauti kwa Kocha Hemed Suleiman (Morocco) ambaye ndiye Mwalimu wa kikosi cha Zanzibar Heroes kilichopo nchini Kenya kikishindana katika mashindano ya CECAFA senior Cup, ambapo alimjumuisha Sangula katika kikosi hicho lakini akaamuwa kutumia kama beki ya kulia badala ya beki ya katikati ambayo ndio nafasi anayotumikia katika timu yake ya Jang'ombe Boys na ndio nafasi iliyompatia jina la Sangula na kumpatia umaarufu Tanzania nzima hata kuvifanya vilabu vya nje ya Zanzibar kufunguwa mazungumzo naye kutaka kumtumia katika vilabu vyao.
Wengine walimbeza kocha Morocco kwa maamuzi yake ya kumtumia Sangula katika nafasi ya ulinzi wa pembeni, lakini majibu ya kocha Morocco yalikuwa "Namuamini na anaweza", wengine walimshawishi Sangula kwamba bora azungumze na Mwalimu ambadilishe nafasi kwa sababu huko anakomchezesha atampoteza kiuchezaji na atashusha kiwango chake, lakini kwa sisi washauri wake, tulimwambia tunza nidhamu yako msikilize Mwalimu wako ona kwamba mbali ya kucheza kuwemo tu katika kikosi cha timu ya Taifa lako hio ni heshima kwako, kwa kuwa Sangula ni msikivu alitusikiliza.
Katika mchezo wa awali dhidi ya Rwanda ambapo Zanzibar ilishimda 3-1 Sangula alianza katika kikosi cha kwanza na akacheza dakika zote 90+, na hapo ndipo Sangula alianza kuwashangaza wale waliombeza kocha Morocco na kumdharau Sangula katika nafasi hio, lakini hata hivyo hawakukosa la kusema ili kutetea hoja yao ya kuwa Sangula hafai kuchezeshwa nafasi hio na walisema kwamba Rwanda hawakuwa wazuri ndio mana Sangula hakupata tabu, lakini subiri siku Zanzibar ikicheza na Tanzania bara kama Sangula hakutolewa kwa 'kash kash' za Shiza Kichuya.
Mwenyezi Mungu akajaalia siku ikafika, siku ya leo ndio mchezo huo ukachezwa kilichotokea sio cha siri kila mtu anakijuwa, awe mwanamichezo au asiwe, awe Bubu, kiziwi, kipofu, wagonjwa wa akili na makundi yote ya jamii Tanzania nzima wanaelewa kwamba Zanzibar iliendeleza ubabe kuwafunga Tanzania Bara 2-1
Katika kikosi cha Zanzibar Heroes Nahodha wetu Sangula alipangwa tena nafasi ya ulinzi wa kulia na kwa Tanzania Bara Shiza Ramadhani Kichuya alikuwa mzima wa afya na akapamgwa katika kikosi hivyo, sote tunaelewa umahiri wa Kichuya katika kuzikimbia beki za pembeni na mipira, lakini kwa siku ya leo Kichuya alikwaa kisiki na kuonekana kana kwamba sio yeye, alijaribu kutoka kupitia upande wa kulia lakini alikutana na mwiba Sangula na akathibitisha kwamba kumbe upande ule sio sahihi na Salama kwa yeye kupita, na kila anapoelekea alikutana na hali kama ile.
Uwezo mwengine wa Kichuya ni kunyang'anya mipira pale tu beki za pembeni zinapopanda na mipira kuelekea langoni kwao, lakini leo ndio siku Sangula aliyokuwa hana shida wala kizuizi mana alipanda mara nyingi, alimkomba Kichuya Mara kadhaa na kuwafanya watangazaji wa mechi wanaomjuwa kushangaa kwanza kumuona akicheza nafasi ile na jinsi anavyoitendea haki nafasi ile, tena mbele ya wachezaji wa kulipwa.
Pia Sangula alimshamgaza mtangazaji wa Kenya na kumtungia jina jipya (rasta mchicha mchicha) pale aliposhangaa jinsi alivyomfupi na anavyocheza mipira ya Kichwa kushinda wenye vimo virefu, pale aliposema "Namshangaa sana huyu rasta mchicha mchicha, mana ana rasta lakini ni ndogo ndogo, nifupi lakini anacheza mipira ya Kichwa zaidi ya waliowarefu".
Kiwango hicho cha Kepteni wetu, kinathibitisha kwamba yeye ni mlinzi imara katika nafasi yeyote na inathibitisha kwamba Kocha Hemed Morocco ni 'Visionary Coach'.
Pia Sangula alimshamgaza mtangazaji wa Kenya na kumtungia jina jipya (rasta mchicha mchicha) pale aliposhangaa jinsi alivyomfupi na anavyocheza mipira ya Kichwa kushinda wenye vimo virefu, pale aliposema "Namshangaa sana huyu rasta mchicha mchicha, mana ana rasta lakini ni ndogo ndogo, nifupi lakini anacheza mipira ya Kichwa zaidi ya waliowarefu".
Kiwango hicho cha Kepteni wetu, kinathibitisha kwamba yeye ni mlinzi imara katika nafasi yeyote na inathibitisha kwamba Kocha Hemed Morocco ni 'Visionary Coach'.
Maoni
Chapisha Maoni