Nahodha wa Jang'ombe Boys ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Ibrahim Mohammed (Sangula) iliyoko nchini Kenya ikisubiria kuanza mchezo wake wa mwanzo wa mashindano ya CECAFA Senior Cup dhidi timu ya Taifa ya Rwanda, amewataka Wazanzibari wote waungane kwa pamoja kuiombea dua timu yao ushindi.
Abdul S
wamad Kassim (Hasgut)
Kwa niaba ya wadau wote wa matandao huu tunaitakia ushindi timu yetu ya Zanzibar Heroes katika mchezo wa leo dhidi ya Rwanda - Amiin.
Ibrahim Mohammed (Sangula)alipokuwa na timu
ya Kombaini Wilaya ya Mjini
Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu Sangula amesema katika maisha kitu chochote cha pamoja hakitafanikiwa endapo wale wanaounda umoja huo pamoja na wadau wa umoja huo hawatakuwa pamoja.
"Hii ni timu ya taifa ya Zanzibar, hivyo tunapaswa kuwa pamoja kwa hali zote, wenye uwezo wa mali na fedha wameshaonyesha kuunga mkono umoja huu kwa kutoa fedha vifaa na vitu vyengine na naamini wataendelea endapo tukifanya vyema, wenye nasaha, maoni na mawazo tayari wametoa maoni, nasaha na mawazo yao kwetu sisi wachezaji na kwa benchi letu la ufundi na naamini wataendelea punde mechi ya leo itakapomalizika.
"Hivyo niwanasihi na wale wanaojiona hawana mchango wowote katika hio niliyoitaja, wasione kama hawana mchango, kila Mzanzibari ana mchango katika timu yake ya taifa na katika mambo yote ya kitaifa na ya kijamii, sio lazima utoe mchango wenye kuonekana, ukituombea dua tucheze salama na ukituombee kimyakimya au kwa dhahiri basi huo ni mchango mkubwa sana na inawezekana mchango wako ukawa ndio mkubwa zaidi kuliko waliotoa mchango unaoonekana.
"Hivyo Wazanzibari wenzangu tuungane kwa pamoja katika hili kwa sababu hili jambo letu sote, na jambo la pamoja linahitaji ridhaa ya wadau wote wa umoja huo, hivyo tuwe kitu kimoja ili kulivuusha jahazi letu leo katika mchezo wa leo dhidi ya Rwanda na michezo yote iliyobakia katika kundi, ili tusonge mbele, alisema Sangula.
Akizungumzia kuhusu mchezo wa leo, Sangula amesema kwamba cmhezo wa leo ni mgumu sana, kutokana na historia ya timu hizo mbili zinapokutana.
"Kiukweli ukiangalia historia, mchezo wa leo ni mchezo mgumu sana, kwa sababu historia ya haraka haraka ni kwamba tumekuwa tukipata ushindi tunapocheza na Rwanda, nilijaribu kuuliza wadau wa miaka ya nyuma na kutwambia kwamba tumeshawafunga Rwanda miaka ya 90 na hata 2012 katika mashindano kama haya kule Uganda tuliwafunga na inasemekana tukikutana na hawa jamaa huwa patashika nguo kuchanika.
"Hivyo timu nzima tunatambuwa hilo, na tutafanya juu chini ili tuzirejee historia hizo, muhimu ni dua zenu na kutuunga mkono, tunashukuru badhi ya Wazanzibari waliopo huku Kenya wanakuja kutuunga mkono mazoezini na hata hotelini wanakuja, hivyo niwaombe wote waje uwanjani pia kutuunga mkono. Alimalizia Sangula
Katika mchezo wa leo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kocha Hemed Suleiman (Morocco) Sangula amepangwa kucheza beki nambari mbili katika kikosi kitakachopambana na Rwanda saa nane adhuhuri ya leo tarehe 05/12/2017.
Kikosi kinachotarajiwa kucheza leo ni kama ifuatavyo:
Mlinda Mlango:
Mohammed Abrahman (Wawesha)
Walinzi:
Ibrahim Mohammed (Sangula)
Haji Mwinyi Mngwali.
Abdulla Kheri (Sebo)
Issa Hidar Dau (Mwalala)
Viungo:
Abdul Aziz Makame (Abui)
Mohd Issa (Banka)
Mudathir Yahya
Feisal Salum (Fei toto)
Washambuliaji:
Ibrahim Hamad Hilika
Suleiman Kassim (Seleembe)
Wachezaji wa akiba:
Ahmed Ali (Salula)Ibrahim AbdallahAdeyum SalehAbdullah Haji (Ninja)Abdul S
Seif Rashid (Karihe)
Kassim SuleimanHamad MshamataKhamis Mussa (Rais)Amour Suleiman (Pwina)Kwa niaba ya wadau wote wa matandao huu tunaitakia ushindi timu yetu ya Zanzibar Heroes katika mchezo wa leo dhidi ya Rwanda - Amiin.
Maoni
Chapisha Maoni