Wachezaji wa timu ya Zanzibar Heroes wameawataka Wazanzibar kuondoa Khofu katika mchezo wa leo dhidi ya Kilimanjaro Star, baadhi ya wachezaji ambao mtandao huu ulizungumza nao kwa njia ya simu ni Khamis Mussa (Rais) na Ibrahim Hamad Hilika ambao wamo katika kikosi cha Zanzibar Heroes kitakachopambana na timu ya taifa ya Tanzania bara (The Kilimanjaro Stars) katika mashindano ya CECAFA Senior Cup 2017 yanayoendelea nchini Kenya.
Kwa upande wa mshambuliaji Khamis Mussa (rais) amewatoa hofu Wazanzibari na wadau wote kwamba siku ya leo timu itashinda bila wasiwasi, na waondoe khofu kabisa.
"Siku ya leo kila Mzanzibari awe na 'Confidence' kwa sababu wachezaji wote nyuso zao zinang'ara kuonyesha kwamba ushindi upo kwetu kwa asilimia kubwa, hivyo wajiamini sana katika siku ya leo" Alisema 'Rais'.
Kwa upande wa Mshambuliaji Ibrahim Hamad Hilika amesema ana matumaini makubwa ya kushinda mchezo wa leo na amewataka Wazanzibar wasiwe na hofu na mchezo wa leo na wasiogope kabisa majina ya Timu ya Tanzania bara.
"Tunataka kuunyesha ulimwengu kwamba sisi tuna uwezo wa kupambana na mtu yeyote licha ya kutuvua uanachama wa CAF, hivyo Wazanzibar na wadau wetu, msiwe na khofu siku ya leo na mechi itakuwa nyepesi sana kwetu, na msitishike na majina ya Tanzania Bara, yale ni majina tu lakini sote tuna uwezo unaolingana au hata tunaweza kuwa zaidi ya wao, ni mazingira tu ndio yanayowafanya waonekane bora, lakini kiuhalisia haiko hivyo, muhimu tuaminini kama mlivyotuamini mchezo wa mwanzo na msiache kutuombea dua". alisema hilika.
Zanzibar Heroes itapambana na Kilimanjaro Stars jioni ya leo, ambapo Zanzibar Heroes wanahistoria nzuri ya mashindano hayo, mwaka 2012 timu hizi zilitoka sare 1-1 katika hatua ya kutafuta mshindi wa tatu kule Uganda na hatimae Zanzibar ikainyuka Kilimanjaro kwa mikwaju ya penalti 6-5.
Khamis Mussa 'Rais'

Ibrahim Hamad Hilika akiwapita Simon Msuva na Haji Mwinyi, wakati Yanga na Zimamoto zilipokutana katika Kombe la Mapinduzi mwaka juzi
Kwa upande wa Mshambuliaji Ibrahim Hamad Hilika amesema ana matumaini makubwa ya kushinda mchezo wa leo na amewataka Wazanzibar wasiwe na hofu na mchezo wa leo na wasiogope kabisa majina ya Timu ya Tanzania bara.
"Tunataka kuunyesha ulimwengu kwamba sisi tuna uwezo wa kupambana na mtu yeyote licha ya kutuvua uanachama wa CAF, hivyo Wazanzibar na wadau wetu, msiwe na khofu siku ya leo na mechi itakuwa nyepesi sana kwetu, na msitishike na majina ya Tanzania Bara, yale ni majina tu lakini sote tuna uwezo unaolingana au hata tunaweza kuwa zaidi ya wao, ni mazingira tu ndio yanayowafanya waonekane bora, lakini kiuhalisia haiko hivyo, muhimu tuaminini kama mlivyotuamini mchezo wa mwanzo na msiache kutuombea dua". alisema hilika.
Zanzibar Heroes itapambana na Kilimanjaro Stars jioni ya leo, ambapo Zanzibar Heroes wanahistoria nzuri ya mashindano hayo, mwaka 2012 timu hizi zilitoka sare 1-1 katika hatua ya kutafuta mshindi wa tatu kule Uganda na hatimae Zanzibar ikainyuka Kilimanjaro kwa mikwaju ya penalti 6-5.
Maoni
Chapisha Maoni