UVUMI WAWA KWELI, JANG'OMBE BOYS VS TAIFA YA JANG'OMBE KATIKA BONANZA LA FUNGA MWAKA

Katibu wa Timu ya Jang'ombe Boys Abdalla Mahfoudh (Dallas) jana amebadilisha uvumi  uliokuwa ukivuma kwa muda wa miezi miwili sasa juu ya uwepo wa mchezo wa maalum wa Bonanza, ambao ni makhsusi kwa kumtafuta mbabe wa Jang'ombe kwa mwaka 2017.

Katibu wa Jang'ombe Boys wa katikati 
akiwa katika majukumu ya timu hio


Na: Ali Mohammed.

Mchezo huo utachezwa tarehe 31/12/2017 saa mbili na nusu za usiku, umetayarishwa na kampuni ya rafikinetwork.net yenye makao makuu yake Mkunazini Kwa Batashi Zanzibar, ambapo kabla ya mchezo huo kutakuwa na matukio ya kiburudani mbali mbali kutengeneza Bonanza hilo.

"Ni kweli timu yetu itacheza mchezo maalum wa kukamilisha Bonanza linaloandaliwa na Kampuni ya Rafiki Network, tulikuwa na mazungumzo takriban zaidi ya mwezi mmoja, mazungumzo hayo yalikuwa ya utatu, yaani mimi niliwakilisha Jang'ombe Boys na katibu wa Taifa ya Jang'ombe aliwakilisha timu yake na timu nzima ya Rafiki netwaork wakiwakilisha kampuni yao.

"Baada ya kipindi chote hicho hatimae sote tulikubaliana kwamba mchezo huo utachezwa tarehe 31/12/2017, kutakuwa na donge nono la zawadi kwa mshindi wa shindano hilo sambamba na kikombe pamoja na nishani, mshindi wa pili pia atapatiwa fedha taslim halikadhalika na medali.

"Niwambie washabiki wa Jang'ombe Boys na wapenda soka kwamba timu hizo zimekuwa zikikutana mara kadhaa, lakini mkutano katika Bonanza hili ni tofauti, kwa sababu ya zawadi nyengine kedekede zitakazotolewa kwa mshindi wa mchezo huo, pia katika michezo yote iliyochezwa kukutanisha vilabu hivi, haijawahi kutokea rais wa nchi hii kufika uwanjani kuangalia timu hizi, lakini kwa heshima na hadhi ya Bonanza na mchezo huu, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein na baraza lake lote na mawaziri watakuepo kiwanjani siku hio.

"Hivyo zawadi zote hizo za kombe, medali, mchezaji bora, kipa bora na za fedha, mwenyewe Dk. Shein ndiye atakaetoa mafurushi hayo ya zawadi kwa timu zote mbili, na niseme kwamba tiketi zimeanza kuuzwa kwa mawakala maalum waliochaguliwa na waandaaji, hivyo nunua tiketi yako mapema kutoka wakala walioidhinishwa zikiwemo timu zenyewe za Jang'ombe Boys na Taifa ya Jang'ombe, na epuka kununua tiketi mikononi,  pia ieleweke kwamba siku ya pambano hilo hakutauzwa tiketi kiwanjani Amani, tiketi zote zinauzwa sasa, pia nitoe indhari, katika Mchezo huu hakutakuwa na ujanja ujanja wowote wa kujaribu kuingia bure kwani milangoni hakutakuwa na walinzi tuliowazoea. Alimalizia Katibu Dallas.

Kwa niaba ya timu na watendaji wote wa Mtandao huu tunawaalika nyote katika mtanange huu maalum wa kumtafuta mkali wa Jang'ombe kwa mwaka 2017.


Maoni