Kitengo cha kuzuia na kupambana na wanamichezo wanaotumia dawa za kutuia nguvu (The World Anti Doping) wakishirikiana na wandaaji wa Mashindano ya CECAFA Serior Challenge Cup yanayoendelea nchini Kenya, leo wamelazimika kuwapima wachezaji wanne wa Zanzibar Heroes kutokana na wasiwasi wa kwamba huenda wachezaji hao wanatumia dawa za kusisimua misuli.
Wasiwasi huo umeelezwa kuwa mwenendo mzuri katika mashindano hayo, kiwango bora ndicho kinachoelezwa kuwa chanzo cha wasiwasi huo uliopelekea vyombo hivyo kuwa na wasiwasi na wachezaji wa Heroes.
Hivyo maafisa wa vyombo hivyo wakawataja wachezaji wanne ambao ndipo macho yao yalipo na wasiwasi, wachezaji hao ni kiungo mchanga Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye ndiye mchezaji bora wa mchezo baina ya Zanzibar na Kenya, Moh'd Issa (Banka), Ibrahim Hamad Hilika na Suleiman Kassim 'Seleembe'.
Hivyo wachezaji hao tayari wameshachukuliwa vipimo na kupelekwa Afrika Kusini kwa vipimo na majibu ya vipimo hivyo yatatolewa baada ya miezi sita ikiwa wanatumia dawa hizo za kusisimuwa misuli au laa.
Endapo ikibainika wachezaji hao kutumia dawa hizo, huenda wakatumikia kifungo cha kutojishughuisha na mpira wa miguu kwa zaidi ya miezi mitatu, adhabu juu ya matumizi ya dawa za kuengeza nguvu michezoni zimewahi ktuolewa kwa wachezaji kadhaa duniani, kama vile mwanariadha Mo Farah, Andrian Mutu wa Chelsea ya uingereza, Rio Ferdinand wa Manchester United na wengineo.
Mshambuliaji Ibrahim Hamad Hilika
akifanyiwa vipimo vya dawa za kusisimua misuli.

Maoni
Chapisha Maoni