Jang'ombe Boys imepata ushindi dhidi ya Miembeni City, ambao ni muhimu sana kutokana na msimamo wa ligi ulivyo, ilionekana tangu mwanzoni kwamba ushindi uliwaelekea vijana wa Jang'ombe Boys kutokana na mpangilio wa mashambuliaji na kasi ya mashambulizi.
Hadi timu zinakwenda mapumziko mchezo ulikuwa 0-0 licha ya Jang'ombe Boys kupata nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia, kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi, ilionekana dhahiri wachezaji waliyafahamu vyema maelekezo ya Mwalimu wao Said Kwimbi, kwani beki za pembeni zilipeleka presha kubwa na kupiga krosi nyingi langoni kwa Miembeni City ambazo zilisababisha kona nyingi.
Alikuwa ni beki wa kati Firdaus Seif (Yobo) wa Jang'ombe Boys aliyeunganisha kwa Kichwa kona muruwa iliyochongwa vyema na Mustafa Vuai (Tafa) aliyesajiliwa msimu huu akitokea timu ya Black Sailors, kona ilipigwa kutokea upande wa kulia wa lango la Miembeni City na kuwafanya washabiki wa Jang'ombe Boys kushangiria goli hilo lililofungwa dakika ya 67.
Ushindi huo basi umeifanya Jang'ombe Boys kuamsha matumaini mema katika ligi kuu ya Zanzibar kwa kufikisha alama 10 na kukwea kutoka nafasi ya 12 ya msimamo hadi nafasi ya 9, huku pengo baina yake na vinara wa ligi hio Black Sailors kuwa ni alama 8, Black Sailors wana alama 18.
Mtandao huu utamzawadia Yobo zawadi maalum kwa kutufungia goli muhimu na la pekee katika mchezo huo.
Mtandao huu utamzawadia Yobo zawadi maalum kwa kutufungia goli muhimu na la pekee katika mchezo huo.
Maoni
Chapisha Maoni