Hatimae michezo ya hatua ya makundi ya CECAFA Senior Challenge cup 2017 imemalizika, na sasa hatua inayofuata ni ya nusu fainali, ambapo timu nne ndizo zilizofuzu hatua hio, timu hizo mbili zinatoka kundi A ambazo ni wenyeji Kenya na Zanzibar na kundi B ni Uganda na Burundi.
Kufuatia hatua hio Zanzibar Heroes imepangiwa kuondoka mji iliopo na kuelekea katika mji wa Kisumu ambao ndio makhsusi kwa shughuli ya hatuwa ya nusu fainali ya mashindano hayo, majira ya saa nane za usiku ndio timu ya Zanzibar Heroes inatarajiwa kupanda ndege kuelekea mjini kisumu ambapo michezo yote ya nusu fainali inatazamiwa kupigwa katika uwanja wa Moi, ambapo katika mchezo wa nusu fainali Zanzibar itapabana na Uganda huku wenyeji Kenya wakipambana na Burundi.
Taarifa iliyotolewa na rais wa CECAFA kupitia Katibu Mkuu wake Bwana Nicholas Muyonye na Makamo wa rais wa shirikisho la mpira wa miguu Kenya Doris Petra zilithibitisha kwamba michezo ya nusu fainali inatachezwa katika uwanja wa Moi Kisumu.
Mtandao huu pia ulizungumza na baadhi ya wachezaji wa Zanzibar Heroes akiwemo Khamis Mussa 'Rais' na Ibrahim Mohammed 'Sangula' ikiwa wana taarifa zozote kuhusu safari hio, na wachezaji waliuthibitishia mtandao huu kwamba mnamo saa nane za usiku watapanda ndege hadi mjini Kisumu ili kusubiria mchezo wao wa Ijumaa kati yao na timu ya taifa ya Uganda (the Cranes) wakiwa ni mabingwa wa tetezi wa mashindano hayo.
Kwa niaba ya mtandao huu, tunawatakia Zanzibar Heroes Safari njema na ushindi katika mchezo dhidi ya 'The Cranes'.
Maoni
Chapisha Maoni