ZANZIBAR HEROES YAFANYA MABADILIKO MADOGO YA KIKOSI KITAKACHOPAMBANA NA KILIMANJARO STARS LEO

Baada ya ushindi mnono na muhimu walioupata Zanzibar Heroes katika mchezo wa awali wa mashindano ya CECAFA Senior Cup 2017 yanayochukuwa nafasi yake kule nchini Kenya, ambapo katika mchezo wa awali Zanzibar iliweza kuinuka juu kwa kuinyuka timu ya Rwanda (Amavubi) kwa magoli 3-1, leo tena itaingia kiwanjani huko Machakos Kenya kusaka alama muhimu ambazo zitaiweka Heroes katika ramani nzuri ya mashindano hayo.


Kikosi cha Zanzibar Heroes KIlichoilaza Rwanda 3-1

Zanzibar Heroes itaingia uwanjani saa nane za mcha a kupambana na ndugu zao Kilimanjaro Stars kutoka Tanzania bara, ambapo Kocha Mkuu wa Zanzibar Heroes ameshaachia hadharani kikosi kitakachoanza leo sambamba na wachezaji 10 wa akiba, katika kikosi hicho kumeonekana kuna mabadiliko madogo sana.

Katika kikosi cha leo Kocha 'Morocco' ameamuwa kumuanzisha Hamadi Mshamata na kumueka akiba Suleiman Kassim 'Seleembe', tofauti na mchezo wa awali ambapo 'Seleembe' alianza na Mshamata kuwa katika wachezaji wa akiba.

Kutokana na mabadiliko hayo pia yamefanya kuwa na mabadiliko ya Nahodha, ambapo mchezo wa awali na Rwanda Nahodha alikuwa 'Seleembe', lakini katika mchezo wa leo nahodha atakuwa Mudathiri Yahya.

Kikosi Kamili ni hichi:

Mlinda Mlango
Moh'd Ibrahim (Wawesha)

Walinzi:
Ibrahim Mohammed (Sangula)
Haji Mwinyi Mngwali
Abdulla Kheri (Sebo)
Issa Haidar (Mwalala)

Viungo:
Abdul Aziz Makame (Abui)
Feisal Salum (Fey toto)
Hamad Mshamata

Washambuliaji:
Ibrahim Hamad Hilika
Mdathir Yahya (Nahodha)
Moh'd Issa (Banka)

Wachezaji wa Akiba:
Ahmed Ali (Salula)
Ibrahim Abdallah
Adeyum Saleh
Abdallah Haji (Ninja)
Seif Rashid (Karihe)
Kassim Suleiman
Suleiman Kassim (Seleembe)
Abdul Swamad Kassim (Hasgut)
Khamis Mussa (Rais)
Amour Suleiman (Pwina)

Tuna haki na wajibu wa kuiombea kila la kheri timu yetu ya Zanzibar Heroes katika mchezo wa leo.

Kwa niaba ya uongozi mzima, washabiki, wadau wa Jang'ombe Boys tunaitakia ushindi mwema na salama timu yetu ya Zanzibar Heroes dhidi ya Kilimanjaro Stars leo.

Maoni