HAWA HAPA 8 WALIOONDOKA JANG'OMBE BOYS NA 8 WAPYA WALIOJIUNGA

Dirisha dogo la usajili ndio hivyo limefungwa, utaratibu wa kikanuni wa kupitisha wachezaji katika vilabu walivyohamia nao halikadhalika umekamilika na kinyume chake ni kusema kuondosha wachezaji katika vilabu walivyohamia nao pia umemalizika.
Mohamad Soud (Makamo wa Rais)



ORODHA YA WACHEZAJI 8 WALIOONDOKA JANG'OMBE BOYS:

1. Ali Humudi Badru (Balii) amehamia Miembeni City.
2. Shomari Said amehamia KMKM
3. Hassan Chum (Mbungi) amehamia KMK
4. Abdahmani Othman (Chinga) amehamia KMKM
5. Ibrahim Novat (Moka) amehamia Malindi
6. Abubakar Mkubwa (Camara) amehamia Villa United
7. Salum Sadi (Sena) amehamia Kilimani City
8. Hafidh Barik (Fiy) amehamia Zimamoto.

ORODHA YA WACHEZAJI 8 WAPYA WALIOSAJILIWA JANG'OMBE BOYS:

1. Bakari Mshenga Vuai amesajiliwa kutoka Danger Boys Chaani
2. Mohamad Soud Foum (makamo wa Rais) amesajiliwa kutoka Good Hope Mkwajuni
3. Mohammed Kipande Yussuf (mchezaji huru)
4. Salum Abdallah
5.Said Yussuf (Kitarabu) amesajiliwa kutoka Mafunzo
6. Bakar Thabit Bakar amesajiliwa kutoka Negro
7. Salum Seif (Bakayoko) amesajiliwa kutoka Miembeni S.C
8. Khatib Ameir Khatib amesajiliwa kutoka Real Kids.

Wachezaji wote hawa waliosajiliwa wameingia katika makubaliano ya mkataba wa miaka mitatu mitatu isipokuwa Bakayoko yeye ameingia miaka miwili pekee, na wote wanahudhuria mazoezi na wote wamehudhuria safari zetu za kimichezo wakati wa mapumziko madogo ya ligi kupisha kombe la mapinduzi.

Jang'ombe Boys ni timu ya mpira yenye viongozi wa mpira inayowatambulisha wachezaji wazuri wasiojulikana na kuwafanya wajulikane na wadau wa mpira wa miguu.

  


Maoni