MANDALIZI YA MCHEZO WA 'DABI' YAKO VIZURI, TAIFA YA JANGOMBE HAWATUWEZI KWA MPIRA NA TUTAENDELEA KUWANYANYASA TAIFA ALHAMIS: RAIS WA JANG'OMBE BOYS

Katika hatua ya kuhakikisha Jang'ombe Boys inaendeleza ubabe wa kuifumua Taifa ya Jang'ombe, Rais wa Jang'ombe Boys Ali Othman (Kibichwa) atema cheche amesema hana wasi wasi na ushindi katika mchezo huo, kutokana na maandalizi yote ya mchezo huo kwenda vizuri, akisungumza na mtandao huu Kibichwa amesema:

Rais Ali Othman kibichwa akizungumza na waandishi wa habari
wakati timu hio ilipofanya kazi ya kijamii kwa kufanya usafi hospitali
ya Kidonge Chekundu.

"Unaweza kufikiria kwamba labda kusingekuwa na maandalizi mazuri na ya kutosha katika mchezo huu kutokana na ughafla wa taarifa za mchezo huu kutoka FA, lakini niseme mchezo huu ndio umepata maandalizi makubwa na ya kutosha kushinda michezo yote ambayo imepita.

"Na hii haikuja bure bali ni kutokana na wadau wote w Jang'ombe Boys kuwa kitu kimoja na kuamuwa kuwekeza mali zao kwa mujibu wa uwezo wao ili kuleta ushindi, ushindi ambao ni furaha na heshima kwetu, sote tunatambuwa Taifa wakitufunga basi huwa hatulali wala hatuli kwa matusi na kebehi, lakini kwa kulitambuwa hilo ndio maana ilipotoka ratiba tu, bila hata kupiga upatu wa kuitisha kikao wanachama na wadau wote walifika kiwanjani na kutaka kujuwa gharama za matayarisho ya mchezo huo na hatimae kuchangia timu yao.

"Hivyo niseme na watu wangu kwamba, hakuna wasi wasi katika mchezo huu, tunakwenda amnai Alhamis kuendeleza rekodi yetu ya kuwanyanyasa Taifa ya Jang'ombe, kwa sababu Taifa hawatuwezi kwa lolote sisi, hawatuwezi kwa uongozi wa mpira, hawatuwezi kwa ubunifu wa mambo ya mpira, hwatuwezi kwa ustaarabu yaani hawatuwezi kwa chochote kinachusiana na mpira wa miguu, wanachotuzidi wao ni uchawi tu, na hilo hatuliogopi wala hatulihofii kwa sababu mpira si uchawi na kama mpira ni uchawi basi Nigeria angekuwa ndiye bingwa wa Dunia. Alimalizia Rais Kibichwa.


Maoni