WACHEZAJI WAPYA JANG'OMBE BOYS WAFURAHIA KUANZA KUITUMIKIA TIMU YAO KWA MCHEZO WA 'DABI' YA JANG'OMBE.

Wachezaji wapya waliosajiliwa na timu ya Jang'ombe Boys wajisikia faraja, fakhari na furaha kuanza kuitumikia klabu yao mpya katika ligi kuu ya Zanzibar kwa mchezo wa 'Dabi' ya Jang'ombe. Kwa nyakati tofauti wachezaji hao wameuambia mtandao huu kwamba baada ya viongozi kutoa taarifa ya uwepo wa  mchezo huo hapo Alhamis ya tarehe 18/01/2018, walijisikia furaha na wenye bahati sana.




Kwa upande wake mshambuliaji mpya wa timu Muhamad Soud Foum aliyesajiliwa kutokea klabu ya Good Hope ya Mkwajuni inayoshiriki faraja la pili Wilaya amesema:

"Unajuwa nimekuwa nikiusikia na naufahamu mchezo wa 'Dabi' ya Jang'ombe kati ya Jang'ombe Boys na Taifa kupitia vyombo vya habari, lakini baada ya juzi kutangaziwa mazoezini kwamba tutacheza mchezo wa mwanzo kuendelea na ligi kuu ya Zanzibar ma Taifa, kiukweli nilifurahi sana, na nikajiona kwamba ni mmoja miongoni mwa wachezaji wenye Bahati sana, kwa sababu nitapata nafasi ya kuonyesha kipaji na uwezo wangu mbele ya mamia ya watazamaji.

" Nawaambia washabiki wangu na washabiki wa Jang'ombe Boys kwamba, endapo Mwalimu akinipanga kuongoza mashambulizi basi sitawaangusha, na niseme yale walioyaona katika mechi za kirafiki ni rasha rasha tu, mvua kamili ni katika ligi kuu hasa hasa katika huu mchezo wa Dabi na Taifa, kwa sababu nataka nianze kazi kwa historia njema. Alimalizia mshambuliaji huyo Mwenye uchu wa kuzifumania nyavu za timu pinzani.

Mshambuliaji Muhamad Soud ambaye washabiki wa Jang'ombe Boys wameshampatia jina jipya la 'Makamo wa Rais' wakimaanisha kwamba ni msaidizi wa Khamis Mussa (Rais) katika kupachika magoli, katika michezo minne ya majaribio aliyocheza tayari ameshapachika kambani jumla ya magoli 4, ambapo ni sawa na wastani wa kila mchezo mmoja kwa goli moja.

Kwa upande wa golikipa kinda Mwenye umri wa miaka 18 na miezi 9 aliyesajiliwa kutokea klabu ya Danger boys ya Chaani Mkurukuchuni kaskazini anatambulika kwa jina LA Bakari Mshenga amesema, ameipokea heshima hii ya mchezo wa 'Dabi' sambamba na kusajiliwa na Jang'ombe boys kwa furaha na unyenyekevu wa hali ya juu sana.

"Hakika nastahiki kumshukuru Allah na kuushukuru uongozi wa Jang'ombe Boys kwa kumuona nafaa kuidakia timu hii, niseme Jang'ombe Boys ni timu kubwa na hizo ndio ndoto zangu kucheza timu kubwa, hivyo kwanza niwaahidi wadau wote kwamba sitawaangusha na naomba waniamini kwa sababu Mimi Mwenyewe najiamini sana.

" Nataka nifanye vizuri katika kila mechi, kuanzia hii ya 'Dabi' na nyenginezo, kwa sababu Nina malengo ya kufika mbali katika soka, kwa sababu bila ya kufanya vyema hapa basi siwezi kufika kule yaliko malengo yangu" alisema Bakar

Akiuzungumzia mchezo wa 'Dabi' Bakari amesema kwamba kwake yeye ni zaidi ya heshima kucheza mchezo huo, ulizingatia umri wake Mdogo na upya wake klabuni hapo.

"Hii ni zaidi ya heshima kwangu, ukizingatia kila nchi ina sina hii ya mechi (Darby), na kila mchezaji anatamani timu yake iwe na mchezo huu, sasa ukiangali umri wangu na timu ninayotokea iko daraja la chini (Daraja la pili wilaya), sasa leo mimi niambiwe ndiye kipa nitakaedaka mchezo wa 'Dabi', Dabi ambayo kila kona ya Zanzibar kwa wapenda mpira macho na masikio yao kuelekea huko, hio ni heshima kubwa kwangu. Alisema Bakari.


Maoni

  1. Me naomba niwasemee viongozi na hata wachezaji kwa ujumla kwamba kuna jambo hawakulisema, "kiukweli hakuna anaetaka au kufurahia kufungwa uwanjani na hasa ukizingatia mchezo huu wa trhe 18 mwezi huu, tumeshuhudia mengi ktk maneno yasiyo mazuri akishtumiwa kiongozi na hata baadhi ya wachezaji kwa kutokufanya vzuri ktk baadhi ya mechi,,,, mm naamini KWIMBI hafundishi kwa lengo tufungwe hapana,, bali jitihada zake kuifanya timu inaibuka na ushindi wa point 3 kibindoni,,, mtu yyte wa soka ni yule anaekubali matokeo yyte kabla ya mchezo kuchezwa" hapo maana yangu ni kwamba cc J. Boys tunapaswa kukubali matokeo yyte ila tusiache kupigania points 3 tukiwa mchezoni. Tuache kulaumu viongozi na wachezaji pindi tunapoharibu mchezo.... Ni hayo tu

    JibuFuta
  2. Ahsante Ndugu Said Omar kwa nasaha, bila shaka washabiki na wadau wa Jang'ombe Boys watazingatia nasaha hizo, kwani Jang'ombe Boys ni ya wastaarabu na ni maumbile ya wastaarabu kunasihika

    JibuFuta

Chapisha Maoni