Ni dhana na utamaduni wa muda mrefu uliojengeka kwa wapenda soka wa Zanzibar kuziona timu za kijeshi (Vikosi) kuwa ndio timu bora tangu vikosi hivyo vya SMZ na vile vya Muungano kujiingiza katika michezo hususan mchezo wa mpira wa miguu na kufanya mapinduzi ya mpira Zanzibar kwa kuziondoa katika nafasi za juu timu za mpira za uraiani (mitaani).
Na hilo linathibitishwa na msimu uliomalizika mshindi wa kwanza ni JKU na mshindi wa pili ni Zimamoto, mbali ya hilo pia msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar inayoendelea nao unathibitisha hilo, ambapo timu nne zinazoongoza ligi zote ni timu za vikosi, ambazo ni KVZ, KMKM, JKU na Zimamoto.
Timu hizo zinaongoza ligi kuu, timu zote hizo na zile nyengine za vikosi ambazo haziko katika nafasi za juu za uongozi wa ligi kila moja imeshaifunga timu isiyo za kijeshi (Uraiani), na kuzifanya timu zote za uraiani zinazoshiriki ligi kuu ya Zanzibar kuwa zimeshafungwa na vikosi, nyengine zimeshafungwa zaidi ya mara moja isipokuwa timu moja pekee ndio haijafungwa na timu yeyote ya kijeshi (Vikosi).

Timu pekee ya uraini ambayo haijafungwa na timu hata moja ya kikosi kwa msimu huu ni timu yetu ya Jang'ombe Boys, ambayo imeshukutana na timu za vikosi kwa msimu huu mara 9 ambapo mara saba (7) tulizokutana tumetoka suluhu na mara mbili (2) tumeshinda, angalia timu tulizokutana nazo za vikozi kwa msimu huu wa 2017/18 na matokeo yake:

- Kipanga mzunguko wa kwanza tulishinda 2-1.
- KVZ mzunguko wa kwanza 1-1.
- KMKM mzunguko wa kwanza 0-0.
- Zimamoto mzunguko wa kwanza 0-0.
- JKU mzunguko wa kwanza 1-1.
- Mafunzo mzunguko wa kwanza 1-1.
- Polisi mzunguko wa kwanza 0-0.
- Kipanga mzunguko wa pili 1-0.
- KMKM mzunguko wa pili 1-1.
x
Maoni
Chapisha Maoni