Kocha Msaidizi Issa Othman (Amasha) ametoa pongezi kwa wachezaji wake baada ya kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Kipanga, kocha huyo mwenye hamasa na uzalendo wa hali ya juu ametoa pongezi hizo baada ya mchezo huo ambapo Jang'ombe Boys imeibuka mshindi kwa jumla ya mabao 2-1.
"Hongereni sana wachezaji wangu kwa ushindi katika mchezo wa leo (jana), nina kila sababu ya kuwapongeza kwa sababu ukiangalia tulicheza pungufu uwanjani, lakini wachezaji mkajituma na hatimae tukapata ushindi.
"Wataalamu wa huu mchezo wanasema ukitaka kuiona timu nzuri, basi ni pale timu hio inapopata mazingira magumu uwanjani na ikapambana nayo na hatimae timu hio ikapata ushindi, basi hio ndio timu nzuri, na wale wachezaji wa timu iliyopata mazingira wakafanya mpaka wakapata ushindi, hao ndio wachezaji wazuri.
"Sasa sifa hizi zisiwalenye, bado tunasafari ndefu ya ligi na ligi inahitaji mazoezi hivyo tunahitajika kufanya mazoezi kwa bidii kama tulivyofanya kabla ya mchezo huu, tushikamane tuwe wamoja kama tulivyoutafuta ushindi huu kwa pamoja, tukifanya hivyo hii ligi nyepesi sana" alisema Amasha.
Jang'ombe Boys kwa sasa iko chini ya kocha msaidizi Amasha, huku ikimsubiri Kocha wake wa zamani raia wa Uturuki Memic Vurugu kuwasili tena Zanzibar kuja kuchukuwa nafasi ya Kocha Mkuu mstaafu Saidi Omar 'Kwimbi' aliyeuomba uongozi wa Jang'ombe Boys kujienguwa katika nafasi hio.
Maoni
Chapisha Maoni