MTAZAMO KATI YA JANG'OMBE BOYS NA BLACK SAILORS KESHO


JEE MAZINGIRA YA USHINDI YAPOJE?
Kwa wadau wakweli wa mpira watakubali kwamba timu yetu kwa sasa iko katika kiwango cha juu cha uchezaji na umiliki wa mpira kila inapokutana na timu yeyote kiwanjani, tatizo ni moja tu kupoteza nafasi nyingi za kushinda magoli, tumecheza michezo yote miwili dhidi ya Kipanga, mpra mzuri umechezwa kwa vipindi vyote, mchezo wa kwanza tumeshinda goli 2-1, mchezo wa pili tumewafunga goli 1-0, mchezo dhidi ya KMKM ulikuwa mzuri na wa kuvutia, tumetengeneza nafasi nying lakini ndio hivyo tumekosa magoli kiajabu ajabu kitendo kilichopelekea kuambulia 1-1.

lakini kwa marekebisho na masahihisho aliyoyafanya mwalimu na morali ya timu iliyoimarika sina shaka mchezo huu utakuwa ni wetu, tamaa ya ushindi ni kubwa sana.

TAARIFA ZA VILABU
Kutokana na kiwango chetu cha kutisha wenzetu wamemua kuukimbia mji kwa wiki nzima sasa na kuweka kambi katika kijiji cha Kizimkazi, wakiamini watapata muda wa kutosha katika kujipanga na kupambana makamanda wa Jang'ombe Boys siku hio ya kesho Alhamis tarehe 01/03/2018 panapo majaaliwa, sisi kama kawaida tupo klabuni kwetu tukiendelea na mazoezi katika kiwanja chetu 'Prizi'.

TIMU ZOTE ZIKOJE MSIMU HUU?
Black Sailors walianza kwa kishindo na hadi kufikia baadhi ya wadau kudhani kwamba wangechukuwa ubingwa mapema sana, waliongoza ligi, walizifunga timu zenye uzoefu katika ligi, lakini baadae ile spidi yao ikashuka baada ya kuonekana wachezaji wao kuchoka na mazoezi mengi na mechi za papo kwa papo (exhaust) na sasa wameshuka hadi nafasi ya 6 wakiwa na alama 22 ambapo wao wametuzidi kwa alama 2 na amepitwa na kinara wa ligi KVZ kwa alama 10.

Jang'ombe Boys tulianza ligi kwa kusua sua na hadi kuwafanya baadhi ya watu ati tutashuka daraja, lakini baada ya kufanya usajili ulioishangaza jamii ya soka, tumeimarika na kuonekana tishio kwa timu pinzani na sasa tuko katika nafasi ya 8 ya msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar 2017/18.

WACHEZAJI WALIOIMARIKA
Kwa kweli kutokana na kiwango cha timu wachezaji wote wanaleta burdani ya aina yake, ila kuna wachezaji wameimarika na wanafanya mambo makubwa zaidi kiwanjani, ukimuangalia beki inayotumiwa kama namba 2 na namba 3, huwezi amini kama hawa wachezaji sio namba zao walizosajiliwa kuchezea, Mansour Marzouk huyu ni mshambuliaji lakini tangu aanze kucheza namba mbili amekuwa mchezaji mzuri sana, ni mlinzi imara anaekimbia sana na ni mwepesi kuziba nafasi,
Juma Moh'd (Mess) huyu ni kiungo mshambuliaji, lakini langu alipoanza kucheza beki nambari 3 khatari sana utadhani amezaliwa kutumikia nambari hio.

Khamis Mussa (Rais -  Machakos), huyu hakuna asiyejuwa uwezo wake, ukimkalia anakufunga ukimuacha anakumaliza, Firdaus Seif (Yobo) huwezi amini amekuwa na kiwango cha juu sana, awali kabla ya kuanza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza alionekana ni beki wa kawaida asiyejiamini wala kuaminika, lakini kwa sasa amekuwa beki wa kutumainiwa sana, Ibrahim Mohammed (Sangula) amekuwa na kiwango kisichoshuka kwa muda mrefu sasa, Khatib Mess ni kijana mdogo lakini anapoingia kutokea benchi hubadilisha aina ya mchezo anakimbia sana na anatoa pasi zenye macho.

Mohamadi Soud (Lukaku), pamoja na kuwa bado hajafunga goli katika ligi kuu ya Zanzibar tangu asajiliwe katika dirisha dogo, lakini ni mchezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji katika kutengeneza mshambulizi, amekuwa akizisumbua beki za timu pinzani na kupiga mashuti mengi sambamba na kutoa pasi za mwisho uhakika.

Mustafa Vuai (Tafa), dah! hakika yupo 'on peak', anakimbia na mipira, anapiga mashuti, anatoa pasi muruwa, amebadilika sana awali alionekana kusua sua na kutokujiamini lakini sasa ameimarika sana.

Hawa ni wachache niliowataja, lakini timu kiujumla imeimarika na imekuwa ni timu isiyofungika ingawa upande wa pili wa shilingi pia huwa tunapata ushindi mgumu sana, lakini hii inachangiwa na kukamiwa na timu pinzani kutokana na uwezo wa msimu uliomalizika.

MATOKEO YA MWISHO DHIDI YA BLAK SAILORS
Mchezo uliopita kati ya pande ulichezwa mwezi Oktoba 2017. Na matokeo yaliwapendelea Black Sailor, tulifungwa 1-0  katika kiwanja cha Amani mchezo ulionekana kama kwamba ungetoka suluhu lakini ni mchezaji Abas Peter John wa Black Sailors kwenye dakika ya 75 akafunga goli la kuongoza na hadi firimbi ya mwisho inapulizwa Black Sailors 1-0 Jang'ombe Boys.

NANI MUAMUZI WA MCHEZO HUU? (REFEREE)
Rashid Msomali, ndio anatarajiwa kusimamia mchezo huu, ni kijana mdogo ambaye ana malengo ya kufika mbali katika fani hii, amewahi kuchezesha michezo kadhaa kwa timu yetu, iko ambayo tumeshinda, iko tuliofungwa na hata kutoka sare.

Sina shaka nae katika utekelezaji wa majukumu yake, ibakie kwamba kila binadamu anamapungufu ya kibinadamu na makosa madogo madogo katika mambo kama haya na mengineyo hayaepukiki, lakini ni mategemeo yangu atasimama imara na kwa uweledi alionao kutenda haki.

HITIMISHO
Mchezo wa mpira una matokeo makuu matatu ambyo ni kushinda, kufungwa, na kutoka suluhu, lakini matokeo yote hayo yanategemea na jinsi timu ilivyojipanga na mchezo husika, jinsi walimu wanavyoifundisha timu nii mani yangu timu yetu ndio itaibuka washindi katika mchezo wa kesho.

Hatuidharau Black Sailor kutokana na kushuka kwa kwango chao na tuniheshimu kwa sababu inatupa tabu sana kuifunga, lakini najengeka imani kutokana na aina ya upambanaji wa vijana wetu, na hicho ndicho kitu pekee kinachonipa matumaini ya ushindi.







Maoni