TUTAWAFUNGWA KMKM.

Jang'ombe itajitupa tena kiwanjani tarehe 22/02/2018 saa 10.00 alaasiri kucheza mchezo wake mwengine wa ligi kuu kusaka alama tatu muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi, mchezo huo utakuwa ni kati yake na timu ngumu ya KMKM, ambayo ni ya Kikosi Maalum cha Kuzuia magendo.

Lakini historia ya hivi karibuni inawabeba Jang'ombe Boys, kwani takriban timu zote za uraiani zimeshafungwa na timu moja au zaidi, isipokuwa ni Jang'ombe Boys pekee ndio timu ambayo haijaonja adhabu za maafande wa vikosi hivyo vya SMZ na vile vya Serikali ya Muungano wa Tanzania ambavyo vinashiriki ligi kuu ya Zanzibar kwa msimu wa 2017/18.

Kumbukumbu zinaonyesha matokeo yafuatayo tuliyoyapata dhidi ya timu za kijesho:

  • Mechi dhidi ya Kipanga mzunguko wa kwanza tulishinda 2-1
  • Mechi dhidi ya KVZ mzunguko wa kwanza tulitoka sare 1-1
  • Mechi dhidi ya KMKM mzunguko wa kwanza tulitoka sare 0-0
  • Mechi dhidi ya Zimamoto mzunguko wa kwanza sare 0-0
  • Mechi dhidi ya JKU mzunguko wa kwanza sare 1-1
  • Mechi dhidi ya Mafunzo mzunguko wa kwanza sare 1-1
  • Mechi dhidi ya Polisi mzunguko wa kwanza sare 0-0
  • Mechi dhidi ya kipanga mzunguko wa pili tulishinda 1-0

Kwa takwimu hizo zinaonyesha dhahidi kwamba timu za vikosi uwezo wao ni mdogo kutufunga msimu huu, ambapo takriban michezo yote nane na timu hizo hakuna hata mmoja ambao tumefungwa na timu hizo zaidi ya sisi kushinda michezo miwili katika hio nane ambapo tumeweza kuwafunga Kipanga mara mbili, ambapo mzunguko wa kwanza tumewafunga goli 2-1 na mchezo wa pili tukawafunga 1-0.

Hivyo washabiki wetu fikeni mapema Insha Allah katika kiwanja cha Amani muje kushuhudia mtanange huo unaotarajiwa kuwa safi na wa kuvutia uliojaa ushindani wa hali ya juu.

Tunaitakia kila la kheri timu yetu - Amiin.








Maoni