Wengi walitaharuki baada ya kumuona mchezaji Yakoub Amour kushindwa kuendelea na mchezo na kulazimika kutolewa nje kwa kitanda maalum cha kubebea wagonjwa mahututi, hivyo tumeona ni vyema tuwape taarifa ya maendeleo ya mchezaji huyo.
Mchezaji kinda wa Jang'ombe boys Yakoub Amour ambaye ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi mbali mbali anaendelea vyema, Yakoub ambaye aliumia katika mchezo wa Alhamis ya tarehe 22 Feb 2018, baada ya kuchapwa daluga na mchezaji wa KMKM Abrahman Othman (Chinga) juu kidogo ya kifundo cha mguu wake wa kulia na kulazimika kutolewa kiwanjani kwa machera.
Kwa mujibu wa katibu wa timu Abdalla Mahfoudh (Dalas) daktari amethibitisha kwamba Yakoub hakuumia sana isipokuwa uvimbe ndio uliosababisha maumivu makali, kitu ambacho kilimsababishia ashindwe kuendelea na mchezo siku ile.
"Kwa kweli madaktari wamesema hakuumia sana sipokuwa kiatu kilimgonga moja kwa moja katika mfupa wa ugoko sehemu ambayo hakukua na kinga (chin guard), lakini hajavunjika mfupa kama tulivyofikiria awali, na asubuhi ya jana alianza kuufanyia mazoezi madogo madogo ufukweni huku akiendelea kupata maelekezo ya kidaktari, na hata jioni jana alifika kiwanjani kuja kuangalia mazoezi, hivyo hali sio mbaya baada ya siku mbili tatu atarudi kuungana na wenzake kufanya mazoezi ya pamoja" alimalizia katibu Dalas.
Mchezo huo ulimalizika suluhu ya goli 1-1.

Maoni
Chapisha Maoni